29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

KUELEKEA OLIMPIKI RIO 2016: Mwanariadha Fabiano aiangukia Serikali

Fabiano Joseph (katikati).
Fabiano Joseph (katikati).

NA WINFRIDA NGONYANI, DAR ES SALAAM

MMOJA wa wanariadha wa mbio ndefu ‘Marathon’ watakaoiwakilisha Tanzania katika michezo ya Olimpiki itakayoanza Agosti 5-21 jijini Rio de Jeneiro, Brazil, Fabiano Joseph, ameitaka Serikali kutoka haraka kiasi cha Sh milioni 80 kwa ajili ya safari yao.

Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Filbert Bayi, kusema kuwa hadi sasa Serikali haijawajibu ombi lao la bajeti ya safari hiyo iliyowasilishwa kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu kutoka Ilboru, Arusha ambako ameweka kambi kujifua kwa maandalizi ya michezo hiyo, Fabiano alisema yeye binafsi anasikitishwa na kitendo cha Serikali kukaa kimya juu ya jambo hilo.

“Mimi naendelea kufanya mazoezi kujiandaa na safari lakini hadi sasa nimekuwa nikijikuta nakata tamaa baada ya kuona Serikali hadi sasa haitusapoti, hivyo ningependa kuchukua fursa hii kuiomba Serikali itoe haraka fedha hizo kutuondoa wasiwasi,” alisisitiza mwanariadha huyo.

Fabiano ataambatana na wenzake  watatu ambao ni  Saidi Juma Makula, Alponse Felix Simbu na Sara Ramadhani Makera, wote kwa pamoja wamefuzu vigezo vya kushiriki michezo hiyo ya kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles