23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Demba Ba asisitiza kuendelea na soka

Demba Ba
Demba Ba

SHANGHAI, CHINA

ALIYEKUWA nyota wa klabu ya Chelsea na Newcastle, mshambuliaji, Demba Ba, amesema hawezi kuachana na soka japokuwa amepata ajali mbaya ya kuvunjika mguu.

Nyota huyo ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini China, Shanghai Shenhua, alivunjika mguu kwenye mchezo wa Ligi Kuu katika dakika ya 64 ya mchezo huo, huku timu yake ikishinda mabao 2-1.

Mchezaji huyo inadaiwa kwamba amevunjika vibaya hivyo inaweza kuwa ni mwisho wa maisha yake ya soka.

Hata hivyo, mchezaji huyo amesisitiza kuwa hawezi kuachana na soka japokuwa ameumia vibaya, ila soka ni sehemu ya maisha yake.

Mchezaji huyo kwa sasa yupo hospitali mjini Shanghai na ameweka wazi kuwa ameumia vibaya lakini anaamini atapona na kuwa sawa kama ilivyo awali.

“Ni kweli nimeumia vibaya, lakini ninaamini hali yangu itakuja kukaa sawa, siwezi kusema kuwa huu ni mwisho wangu wa maisha ya soka, nina uhakika nitaendelea kucheza soka.

“Nilitakiwa kufanyiwa upasuaji sehemu yote ambayo nimeumia, lakini nimewaambia madaktari kuwa wasubiri kidogo. Mwenyewe nilitaka niende Ulaya kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji, lakini naona haiwezekani ila nimeongea na daktari hivyo ninatarajiwa kufanyiwa upasuaji na daktari wa nchini Ufaransa.

“Tayari mazungumzo yameanza kufanyika, hivyo daktari huyo anatarajia kuwasili nchini China muda wowote kwa ajili ya kunifanyia upasuaji,” alisema Demba Ba.

Mchezaji huyo kabla ya kuvunjika mguu alikuwa tayari amecheka na nyavu mara 14 katika michezo 18 aliyocheza katika michuano ya ligi hiyo nchini China.

Hata hivyo, anaamini Machi mwakani atakuwa uwanjani katika msimu mpya wa Ligi Kuu nchini humo.

“Kuna wachezaji ambao wamewahi kupata tatizo kama hili, Hatem Ben Arfa aliwahi kuvunjika kama mimi ila ameweza kurudi tena uwanjani, hivyo ninaamini nitakuwa vizuri muda mfupi ujao na ninaamini nitaweza kujiunga na timu Machi mwakani kwa ajili ya msimu mpya wa ligi.

“Kwa sasa ligi yetu inatarajia kumalizika Novemba  mwaka huu, ninaitakia timu yangu iweze kufanya vizuri na kutwaa ubingwa huo,” aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles