25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Hakuna upungufu wa mafuta nchini – Ewura

Felix Ngamlagosi
Felix Ngamlagosi

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MAMLAKA ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imesema  nchi  ina mafuta ya aina zote ya kutosha na hakuna tatizo linaloonyesha kutokea   upungufu wa mafuta   siku zijazo.

Taarifa hiyo ya EWURA ilitolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Felix Ngamlagosi, ilieleza kuwa nchi ina petroli ya kutosha matumizi ya siku 12, dizeli ya siku 15 na mafuta ya taa siku 16.

Alisema  meli zinaendelea kuingiza mafuta kwa mujibu wa ratiba ilivyopangwa.

Ngamlagosi alisema baadhi ya mikoa hususan Ruvuma na Mtwara, ilikuwa na upungufu wa petroli kutokana na mapumziko marefu ya sikukuu za Saba Saba, Eid el Fitr na     mwisho wa wiki.

“Katika hali hiyo baadhi ya maghala hayafanyi biashara siku hizo. Katika mikoa iliyotajwa, wateja walipata wasiwasi wa uhaba wa mafuta na kununua kwa wingi, jambo ambalo liliongeza tatizo.

“Hata hivyo, mikoa ya Ruvuma na Mtwara imeendelea kupokea mafuta ya aina zote tangu Julai 8, mwaka huu  na hali ya soko inaendelea kutengamaa.

“EWURA inawasihi watumiaji wa mafuta ya jamii ya petroli kutokuwa na wasiwasi na waendelee kununua kwa utaratibu wa kawaida,” alisema Ngamlagosi .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles