MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani, Amber Rose, anatarajia kumwalika baba mtoto wake katika kipindi chake cha Amber Talk Show.
Mrembo huyo amedai kwamba atakuwa na furaha kubwa kumkaribisha mume wake wa zamani katika kipindi hicho kwa ajili ya kuelezea maisha yake.
Hata hivyo, kupitia akaunti yake ya Instagram, Wiz Khalifa amedai kwamba hatakuwa na mengi ya kuongea kama watu wanavyodhani.
“Nitaenda kupita tu, sitokuwa na muda wa kupoteza, lakini nashukuru sana kwa kunipa nafasi hiyo kuwa mgeni rasmi,” aliandika Wiz Khalifa.
Wawili hao walifanikiwa kupata mtoto wa kiume na kumpa jina la Sebastian, lakini baada ya muda waliachana.