MKALI wa muziki wa RnB, Jason Derulo, ameachana na mpenzi wake, Daphne Joy baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa miezi saba.
Msanii huyo alianza uhusiano na mwanamitindo huyo baada ya kuachana na rapa 50 Cent aliyezaa naye mtoto mmoja anayejulikana kwa jina la Sire mwenye umri wa miaka mitatu.
Hata hivyo, hadi sasa haijawekwa wazi chanzo cha wawili hao kuachana lakini mashabiki wamedai kwamba wawili hao wameachana kutokana na mrembo huyo kumzidi umri Derulo ambaye ana miaka 26, huku Daphne akiwa na umri wa miaka 29.