25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Hali si shwari Simba

5NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

HALI si shwari tena ndani ya klabu ya Simba baada ya Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo kuanza kusambaratika na wachezaji wa kimataifa kugomea kusafiri na timu kwenda Songea kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Majimaji.

Jana Mjumbe wake wa Kamati ya Utendaji, Idd Kajuna, alibwaga manyanga. Kajuna ameamua hayo siku chache baada ya Simba kushindwa kutwaa ubingwa wa ligi, huku ikipata matokeo mabaya katika mechi za kumaliza msimu wa 2015/16.

Simba juzi ilijiondoa rasmi kusaka ubingwa huo, baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 mbele ya Mwadui FC, hivyo kuwasafishia njia Yanga ya kuchukua kombe hilo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kajuna alisema anatarajia kuwasilisha barua ya maamuzi yake hayo kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji ili kupata ridhaa yao, ambapo atabaki kama mwanachama wa kawaida.

“Leo (jana) tutakuwa na kikao cha kamati, ambapo wajumbe wote tumetakiwa kuhudhuria na kupitia kikao hicho ndio nitawasilisha maamuzi yangu hayo ili kupata ridhaa yao,” alisema.

Alisema kwa sasa yupo mkoani Mbeya kwenye biashara zake lakini hadi jioni atakuwa amewasili Dar es Salaam na kuhudhuria kikao hicho.

Maproo wagomea timu

Wachezaji wa kimataifa wa Simba, wanadaiwa kugomea kujiunga na wenzao katika safari ya kuelekea Songea kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Majimaji unaotarajiwa kuchezwa kesho  Uwanja wa Majimaji.

Mgomo wa wachezaji hao unadaiwa kusababishwa na madeni ya mshahara wanayoidai timu hiyo ambapo mdhamini mkuu wa timu hiyo Bia ya Kilimanjaro bado hajatoa fedha hizo.

Meneja wa timu hiyo, Abbas Ally, alikiri kukosekana kwa baadhi ya wachezaji kwenye safari hiyo, lakini hakuweka wazi ni kina nani.

“Baadhi yao wapo na wengine hawapo,” alisema hivyo na kusita kuwataja waliokuwepo na waliokosekana.

Wachezaji hao ni Justice Majabvi, Vicent Angban, Emery Nimubona, Hamis Kiiza, Juuko Murshid na Mwinyi Kazimoto ambao wanadaiwa watajiunga na timu leo hii.

 

Wakati huo huo habari za uhakika zilizolifikia gazeti hili, zimesema kuwa vigogo wengine wa Simba wakiongozwa na Makamu wa Rais, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ na Saidi Tully, wamekalia kuti kavu baada ya kushutumiwa zaidi na mashabiki kuhusika na sakata la kuihujumu timu.

“Viongozi hao nao wana asilimia chache za kuendelea kuiongoza Simba, kutokana na mashabiki kuwatuhumu mara kwa mara, lakini pia mchezaji Hamis Kiiza naye yupo kwenye hatari ya kuachwa,” alisema.

Kaburu asakwa na mashabiki

Katika hatua nyingine juzi baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Mwadui FC, baadhi ya mashabiki walijipanga nje ya geti na kufanya msako kwenye kila gari linalotoka ili kuangalia kama kiongozi huyo amejificha.

Mashabiki hao waliokuwa wakisema kuwa wanamtaka Kaburu, walilazimisha kila gari kusimama na kuwataka madereva wafungue buti ili waangalie kama hajajificha humo.

Kioo cha basi la Simba chavunjwa

Hasira za mashabiki hao walizimalizia kwenye basi la Simba, ambapo wakati linatoka walilipiga mawe na kuvunja kioo, lakini hakuna mchezaji aliyejeruhiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles