25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

CCM hatucheki na mtu katika kushika dola, Tumejipanga- CPA MAKALLA.

Na Mwandishi Wetui

KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi, Uenezi, Siasa na Mafunzo CPA Amoss Makalla amesema Chama hicho hakicheki na mtu katika kushika dola na katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu na wamejipanga kuhakikisha wanashinda kwa kishindo.

CPA Makalla ameyasema hayo leo Movemba 23,2024 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji unaotarajia kufanyika Novemba 27 mwaka.

Amesema kuwa kwa sasa Chama hicho kimeendelea kufanya kampeni za Uchaguzi huo na walizindua kampeni zao rasmi Novemba 20 mwaka huu katika mikoa yote nchini na tangu kuanza kampeni hizo wagombea wa Chama hicho wataibuka na ushindi wa kishindo .

“Katika uchaguzi huu wa Serikali ya Mitaa tutashinda na tunataka ushindi wa kishindo.Kwa jinsi ambavyo CCM tumejipanga ni sawa na kusema yanayoendelea ni sawa na kusema yajayo yanafurahisha,”amesema CPA Makalla.

Akisisitiza zaidi amesema uchaguzi huo ni muhimu na CCM inachukulia uchaguzi huo kwa umuhimu mkubwa kwani inatambua kazi ya chama cha siasa ni kushika dola na Chama hicho kinaanza na kushinda uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

“Kazi ya Chama cha siasa kilichosajiliwa ni kuhakikisha kinashika dola maana kazi ya kuhubiri kwenda mbinguni hiyo inafanywa na viongozi wa dini.Kwa kutambua umuhimu wa kushika dola ndio maana katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa CCM imeweka wagombea wake kwa asilimia 100 kwani hakuna Mtaa,Kijiji Wala Kitongoji ambacho tumeacha,kote tumesimamisha wagombea a kwa nafasi zote.

“Vyama vingine havina utayari na ndio maana wameshindwa kusimamisha wagombea katika nafasi zote na mpaka sasa kuna Mitaa ambayo tayari wagombea wake hawana washindani,”amesma CPA Makalla na kuongeza katika maeneo ambayo wapinzani hawajasimamisha wagombea kampeni ziendelee maana kutakuwa na ndio au hapana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles