27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 30, 2024

Contact us: [email protected]

Vyombo vya Habari vyatakiwa kuhamasisha jamii kufanya uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza

Na Mwandishi Wetu

Wahariri wa vyombo vya habari nchini wametakiwa kutumia vyombo hivyo kuihamasisha jamii kufanya uchunguzi wa afya upande wa magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo magonjwa ya moyo.

Rai hiyo imetolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Dk. Tulizo Shemu alipokuwa akizungumzana wahariri hao waliofika kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo katika Kliniki ya JKCI iliyopo Kawe jijini Dar es Salaam.

Dk. Shemu amesema magonjwa ya moyo yanaua kwa kasi hivyo jamii ikiweza kupata elimu ya kutosha ya namna ya kutambua na kujikinga na magonjwa hayo itaweza kuyadhibiti kwa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara kufahamu mapema na kuzuia gharama kubwa za matibabu ambazo mtu angetumia kwa kuchulewa kufanya uchunguzi.

“Magonjwa ya moyo huja kwakushtukiza, zaidi ya asilimia 60 ya watu wanaopata mstuko wa moyo hupoteza maisha kutokana na kuchelewa kupata huduma za matibabu kwa wakati”, amesema Dk. Shemu

Aidha Dk. Shemu ameitaka jamii pale inapokutana na changamoto za maumivu makali upande wa kushoto wa kifua kufika hospitali mapema kwa ajili ya uchunguzi kwani maumivu hayo wakati mwingine hutokana na tatizo la mstuko wa moyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile ameipongeza Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete kwa kuwa na maono ya kuwafikia watu wa aina mbalimbali kuwafanyia uchunguzi wa afya kwani bila hamasa hizo wapo watu ambao hasingepima.

Balile amesema kupitia upimaji huo wahariri zaidi ya 50 wamekutana kwaajili ya kuangalia afya zao ambapo wapo ambao hawakuwahi katika maisha yao kupima kipimo cha moyo hivyo kwao kuwa fursa.

“Kwakweli sisi kama wahariri tumefurahi sana kuona taasisi hii inatujali hivyo kuweka historia kubwa katika maisha yetu kwa kufanya vipimo hivi na kupata elimu ya kuwa tunachunguza afya zetu” amesema Balile

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles