25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Sekta binafsi yapongezwa kwa huduma bora

Na Mohammed Ulongo, Dar es salaam.

Jeshi la Polisi limeeleza kuridhishwa na huduma bora inayotolewa na sekta binafsi ya ulinzi ambayo imesaidia kuendeleza usalama wa raia na mali zao hapa nchini.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Mkuu wa Ushirikishwaji Jamii wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kinondoni ASP Elina Maro wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wateja duniani, iliyoandaliwa na Kampuni Binafsi ya Ulinzi ya G4S ya jijini Dar Es Salaam.

Hata hivyo ASP Elina Maro amezitaka jamii kujiepusha na vitendo vya kumaliza kindugu au kufanya makubaliano katika kesi za jinai kwani kufanya hivyo ni kumnyima haki mlalamikaji wa kesi husika.

Pia ameipongeza kampuni hiyo kwa rekodi nzuri ya utoaji huduma bora kwa wateja wa ndani na nje ya nchi wakiwemo wawekezaji, na kuomba ufanisi huwo uendelea kwa faida ya vijana walioajiriwa pamoja na usalama wa nchi kiujumla.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Ulinzi ya G4S, Imelda Lutebinga amesema ufanisi wa kampuni hiyo iliyosambaa nchini kote na nje ya nchi unatokana na kupokea ushauri na maoni kama mrejesho wa huduma inayotolewa kwa wateja wake.

Pia ameongeza kuwa miongoni mwa huduma zinazotolewa na Kampuni hiyo ni pamoja na ulinzi wa kawaida, usafirishaji wa fedha na huduma nyingine ambazo ni suluhisho kwenye mifumo mbalimbali ya kiusalama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles