26.5 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

PPRA yahimiza wananchi kutumia fursa ya sheria ya manunuzi kujikwamua kiuchumi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti Ununuzi wa Umma (PPRA), Mhandisi Juma Mkobya, amewahimiza wananchi kutumia fursa zinazotolewa na Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2023 ili kujikwamua kiuchumi.

Mhandisi Mkobya alitoa wito huo jijini Mwanza Oktoba 12, 2024 alipokuwa akielimisha wananchi waliotembelea banda la mamlaka hiyo kwenye maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa kuhusu fursa za kiuchumi zinazotolewa na sheria hiyo.

Alibainisha kuwa sheria hiyo inatoa kipaumbele kwa makundi maalum kama vile wazee, vijana, wanawake, na wenye ulemavu. Makundi haya yanahimizwa kuwa kwenye vikundi vilivyosajiliwa katika halmashauri zao na kujisajili katika mfumo mpya wa kielektroniki wa manunuzi ya umma (NEST).

“Serikali inaboresha mazingira ya uwekezaji kwa wazawa kupitia sheria hii, ambayo pia inataka zabuni zote ambazo mtaji wake hauzidi shilingi bilioni 50 ziende kwa wazawa,” alisema Mhandisi Mkobya.

Aliongeza kuwa sheria inawapa kipaumbele wazawa kwa kutamka kuwa, hata kama kampuni ya mzawa ina mtaji mdogo ikilinganishwa na wageni anaoshirikiana nao, lazima mzawa awe kiongozi katika mchakato wa kupata zabuni.

Aidha, alifafanua kuwa Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2023 haina urasimu kwa muombaji wa zabuni, jambo linalorahisisha upatikanaji wa fursa kwa makundi maalum.

Kwa mujibu wa Mhandisi Mkobya, makundi maalum 470 tayari yameshasajiliwa kwenye mfumo wa NEST. Ameeleza kuwa wameitumia Wiki ya Vijana kufikia makundi maalum yaliyotajwa, ili kuhakikisha wanapata manufaa yanayotokana na sheria hii mpya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles