26.6 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Mahakama yaombwa kuruhusu ushahidi kesi ya kujeruhi, lugha chafu

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Katika kesi ya kujeruhi na kutoa lugha chafu inayowakabili wanandoa, Bhartat Natwan (57) na Sangita Bharat (54), upande wa utetezi kupitia Wakili Edward Chuwa umeomba mahakama kuruhusu kuoneshwa kipande cha video kinachoonyesha mlalamikaji, Kiran Ratilal, akitumbukizwa kwenye ndoo ya saruji.

Maombi hayo yaliwasilishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Aaron Lyamuya, wakati kesi hiyo ikiendelea katika Mahakama ya Hakimu-Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, shahidi huyo hakuwa na kipande hicho cha video wakati huo, jambo lililozua maswali kuhusu ushahidi wa tukio hilo.

Wakili Chuwa alihoji kwa nini hakuna shahidi yeyote kutoka kwa zaidi ya wakazi 40 wa eneo la tukio ambaye alijitokeza kushuhudia au kuingilia kati ugomvi huo, isipokuwa msimamizi wa jengo ambaye si mkazi wa eneo hilo. Mashaka haya yaliongeza utata juu ya madai ya mlalamikaji.

Kesi hiyo imechukua mwelekeo mpya baada ya Wakili wa Serikali, Grace Mwanga kubadilishwa na nafasi yake kuchukuliwa na Wakili Faraji Nguka kutoka Dodoma, ambaye sasa ataendelea na uendeshaji wa kesi hiyo.

Wanandoa hao wanatuhumiwa kumjeruhi na kutoa lugha chafu dhidi ya Kiran Ratilal katika tukio linalodaiwa kutokea Julai 21, 2023, katika jengo la Lohana, Mtaa wa Mrima-Kisutu, Dar es Salaam.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena Agosti 30, 2024, saa tatu asubuhi, ambapo mashahidi wengine wa upande wa mashtaka wataendelea kutoa ushahidi wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles