25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

RC Mara apokea wazo la Tuzo kwa Waandishi wa Habari

Na Malima Lubasha, Serengeti

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, ameunga mkono wazo la kuanzisha mchakato wa tuzo kwa waandishi wa habari mkoani Mara. Wazo hili lilitolewa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC) katika mdahalo uliofanyika Julai 5, 2024, mjini Musoma. Tuzo hizi, zinazotarajiwa kuanza kutolewa Desemba mwaka huu, zitalenga waandishi watakaoandika habari za kutangaza sekta mbalimbali na kuvutia wawekezaji mkoani Mara.

Akizungumza kwenye mdahalo huo, Kanali Mtambi amesema kuwa wazo hili ni zuri na litaongeza chachu kwa waandishi wa habari kutangaza fursa zilizopo mkoani Mara. Alibainisha kuwa mkoa wa Mara una fursa nyingi kama Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Ziwa Victoria, madini, mifugo, na makumbusho ya Mwalimu Julius Nyerere huko Butiama, ambazo hazijatangazwa vizuri.

Mkuu wa Mkoa aliipongeza Klabu ya Waandishi wa Habari kwa kuandaa mdahalo huo na kualika wadau mbalimbali kujadili fursa zilizopo mkoani Mara. Alihimiza kufuatilia utekelezaji wa mawazo yaliyotolewa kwenye mdahalo huo baada ya miezi minne.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara, Mugini Jacob, alishukuru Mkuu wa Mkoa kwa kushiriki na kupokea wazo la tuzo kwa waandishi. Alisisitiza kuwa waandishi wa habari mkoani Mara wapo tayari kushirikiana na ofisi ya mkoa kutangaza fursa za uwekezaji.

Tuzo hizo zitahusisha zawadi ya fedha na cheti kwa waandishi watakaofanya vizuri katika kuandika habari za kutangaza mkoa wa Mara. Wadau kama Nyihita Sunflower, TCCIA, WAMACU, TANROAD, HAIPPA, GRUMETI FUND, na TAWA walizungumza na kutoa mawazo yatakayovutia wawekezaji kuja kuwekeza mkoani Mara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles