Na Barnabas Lugwisha
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania amezindua awamu ya pili ya kampeni ya ‘Mtu ni afya’ juzi Mjini Kibaha Mkoa wa Pwani ikiwa ni mara ya 50 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1973.
Katika hafla hiyo Shule ya Istiqaama ya jijini Tanga ilishika nafasi ya pili katika Mshindano ya Afya na Usafi wa Mazingira kundi la shule za Sekondari Tanzania Bara.
Dk. Mpango alisisitiza umuhimu wa kutunza mazingira na kuendelea kuzingatia kanuni za afya, pia amezipongeza taasisi ambazo zimefanya vizuri katika swala la afya na usafi wa mazingira ambao kwenye kundi la shule za Sekondari Tanzania Bara.
Dk. Mpango ameipongeza shule ya Istiqaama ya jijini Tanga kwa kushika nafasi ya pili shule zilizofanya vizuri zaidi kwa mwaka 2023.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Mohamed Hamad Mohamed, ameupokea ushindi huo kwa furaha na kuahidi kufanya vizuri zaidi kwa mwaka unaokuja.
“Kwa upende wetu usihindi huu ni chachu ya kufanya vizuri zaidi katika mashindano yajayo,” amesema Mohamed.