29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kapombe aanza tiba Afrika Kusini

NA ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM
kapombe3-2BEKI kisiki wa mabingwa wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, Shomari Kapombe, ameanza kupata matibabu ya kifua katika hospitali ya Morningside Mediclinic iliyopo Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Beki huyo tegemeo wa Azam aliondoka juzi baada ya kusumbuliwa na tatizo hilo na hivyo kulazimika kukosa michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kapombe alikosa mechi mbili zilizopita dhidi ya Toto Africans na Ndanda lakini hali ilizidi kubadilika katika mchezo wao dhidi ya Toto Africans ya Mwanza kabla ya kukimbizwa hospitalini.

Daktari wa Azam, Juma Mwimbe, ameliambia MTANZANIA Jumamosi kuwa beki huyo atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki mbili na hivyo kulazimika kuikosa michezo miwili ya kimataifa pamoja na ile ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Kapombe amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya kifua mara kwa mara na  amekuwa akilalamika mbavu zinamuuma hivyo kwa kuwa Azam tunajali hali ya wachezaji wetu, uongozi umeamua kumpeleka Afrika Kusini kupatiwa matibabu na ameanza leo nafikiri kila kitu kitaenda sawa.

“Tunakadiria atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki mbili lakini zinaweza kuongezeka kutokana na ripoti ya madaktari watakayokuja nayo, kiukweli ni pigo kwetu  kwani ni mchezaji muhimu katika kikosi cha Azam,” alisema.

Beki huyo wa zamani wa Simba na AS Cannes ya Ufaransa, amekuwa mmoja wa wachezaji tegemeo wa Azam FC msimu huu kwenye mechi mbalimbali alizocheza na ameifungia timu hiyo jumla ya mabao 11 yakiwemo nane ya ligi.

Mbali na mabao hayo, Kapombe pia amecheka na nyavu mara mbili katika michuano ya Kombe la Shirikisho (FA), huku lingine akifunga katika Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Bidvest Wits walipoichapa mabao 3-0 mjini Johannesburg kabla ya kufuzu raundi ya pili ya michuano hiyo kwa jumla ya mabao 7-3.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles