25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Kinara wa kubebesha wanawake dawa za kulevya akamatwa

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), imemkamata kinara wa mtandao wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya aina ya cocaine nchini ambapo wanawake wanaongoza kubebeshwa dawa hizo kusafirisha maeneo mbalimbali.

Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa DCEA, Aretas Lyimo, mfanyabiashara huyo ana uwezo wa kusafirisha watu 10 maarufu punda, huku wanawake wakiongoza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 25,2024 jijini Dar es Salaam, Lyimo amesema mfanyabiashara huyo aliyekuwa anatafutwa tangu mwaka 2000, amekamatwa maeneo ya Boko jijini humo.

Amesema wamefanikiwa kumkamata akiwa na gramu 692.336 kutokana na oparesheni inayoendelea nchinj kwa sasa.

“Mfanyabiashara huyu wa mtandao wa cocaine ambaye alikuwa anatafutwa mda mrefu kabla ofisi ya DCEA haijafunguliwa ni miaka 23 anatafutwa hivyo alikamatwa katika eneo la Boko Wilaya ya Kinondoni pamoja na washirika wake watatu,”amesema Kamishna Lyimo.

Ameeleza kuwa kati yao wawili walikamatwa jijini Dar es Salaam na mmoja amekamatwa katika Kijiji cha Shamwengo Wilaya ya Mbeya vijijini.

Amesema wasafirishaji huwa wanazimeza zikiwa katika mfumo wa pipi ambapo kwa mara moja mtu anabeba kuanzia gramu 300 hadi 1200 na wengine hadi gramu 2000 kwa wakati mmoja.

Aidha ametangaza oparesheni kali ya dawa za kulevya ya 2024 ambayo itafanyika nchi kavu na baharini katika kumbi za starehe,hoteli za watumia shisha.

Amefafanua kuwa oparesheni ya nchi kavu itahusisha mashamba ya dawa za kulevya kwenye mipaka na maeneo ya mjini kwa upande wa bahari zitahusisha fukwe na katikati ya bahari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles