32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Magufuli awataka Watanzania waliombee Taifa

MaguNa Mwandishi Wetu, Chato

RAIS Dk. John Magufuli amewataka Watanzania wote kuendelea kuliombea Taifa liendelee kuwa na amani.

Kauli hiyo aliitoa jana alipoungana na waumini wenzake wa Kanisa la Bikira Maria Parokia ya Chato kusali Ibada ya Jumapili ya pili ya Pasaka ikiwa ni mara ya kwanza tangu achaguliwe kuliongoza Taifa.

Aliwaomba Watanzania wote waendelee kushirikiana na kushikamana kwa umoja wao na siku zote wamtangulize Mungu.

“Wakati tunaadhimisha wiki moja baada ya kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo  aliyekufa kwa sababu ya dhambi zetu.

“Sisi wote tujitahidi kufuata matendo ya Yesu Kristo ya kusameheana, kupendana, kushirikiana na tusibaguane,”alisema.

Katika ibada hiyo, Rais Magufuli, alichangia Sh milioni 10 kwa ajili ya upanuzi wa kanisa hilo.

Taarifa iliyotolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu, Gerson Msigwa, ilieleza kuwa pamoja na Rais Magufuli na mkewe Janeth,  ibada hiyo pia ilihudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya, Raila Odinga na mkewe Mama Ida Odinga ambao ni familia rafiki wa Rais Magufuli.

Raila na mkewe waliwasili Chato juzi jioni kwa mapumziko.

Katika salamu zake kwa waumini wa Parokia ya Chato, Raila,  aliwashukuru Watanzania kwa uhusiano mzuri  na Wakenya.

Alitoa mfano   jinsi Marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu   Nyerere alivyojitoa kupigania uhuru wa mataifa mengi ya Afrika ikiwamo Kenya.

“Urafiki wetu na Rais Magufuli ulianza tangu alipoteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi na mimi kuwa Waziri mwenye dhamana ya ujenzi Kenya.

“Mara kadhaa tulibadilishana uzoefu na kushirikiana katika mipango ya miradi ya ujenzi wa barabara.

“Kwa umuhimu huo natoa wito kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuendeleza ushirikiano na mshikamano ulioasisiwa na waasisi Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania, Jaramogi Odinga wa Kenya na Milton Obote wa Uganda,” alisema Raila.

Waziri Mkuu huyo mstaafu wa Kenya, alisema  katika kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Kenya, anakumbuka jinsi  Mwalimu   alivyomsaidia kumpa hatia ya kusafiria ya Tanzania  ambayo aliitumia kwenda kusoma nje ya nchi.

Akizungumzia Kuhusu urafiki wake na Rais Magufuli, Odinga, alisema ulianza tangu Rais Magufuli alipoteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi na yeye kuwa Waziri mwenye dhamana ya ujenzi wa Kenya, ambapo mara kadhaa walibadilishana uzoefu na kushirikiana katika mipango ya miradi ya ujenzi wa barabara.

Kutokana na hali hiyo alitoa wito kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuendeleza ushirikiano na mshikamano uliojengwa na waasisi wake wakiongozwa na Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

“Urafiki wetu na Rais Magufuli ulianza tangu alipoteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi na mimi kuwa Waziri mwenye dhamana ya ujenzi Kenya.

“Mara kadhaa tulibadilishana uzoefu na kushirikiana katika mipango ya miradi ya ujenzi wa barabara.

“Kwa umuhimu huo natoa wito kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuendeleza ushirikiano na mshikamano ulioasisiwa na waasisi Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania, Jaramogi Odinga wa Kenya na Milton Obote wa Uganda,” alisema Raila.

Rais Magufuli yupo mapumzikoni nyumbani kwake, Lubambangwe katika Kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato mkoani Geita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles