28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Tanzania, Irani zasaini makubaliano

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Tanzania na Jamhuri ya Kiislam ya Iran zimesaini makubaliano ya majadiliano ya kuondoa utozaji kodi mara mbili baada ya kufanyika kwa majadiliano ya kati ya nchi hizo mbili.

Makubaliano hayo yamesaniwa jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera na Utafiti, Wizara ya Fedha, William Mhoja kwa upande wa Tanzania na Mkurugenzi wa Sheria na Mikataba ya Kodi wa Irani, Dk. Hossein Abdallah.

Akizungumza baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, Mhoja amesema kuwa yatahusu misingi ya utozaji kodi ya mapato katika shughuli zinazofanywa na raia, kampuni na taasisi za nchi mojawapo kwenye nchi hizo.

“Makubaliano hayo yanaweka misingi ya ushirikiano katika usimamizi wa kodi kati ya mamlaka za usimamizi wa kodi za nchi hizi mbili kupitia ubadilishanaji wa taarifa za kikodi na kusaidiana kwenye masuala ya kodi, “amesema Mhoja.

Amesema kuwa kusainiwa kwa makubaliano hayo kulianza na majadiliano yaliyofanyika kuanzia tarehe 15 hadi 18 Januari, 2024 jijini Dar es Salaam na kubainisha kuwa yalikuwa ya duru ya tatu kutokana na kushindwa kufikia maridhiano katika duru mbili zilizotangulia.

Mhoja ameeleza kuwa, Tanzania na Iran zina ushirikiano wa kihistoria katika masuala mbalimbli ya kiuchumi hivyo kukamilika kwa majadiliano na kusainiwa kwa makubaliano hayo kutaimarisha zaidi ushirikiano wa kiuchumi kwa kufungua fursa mpya za ajira, biashara na uwekezaji.

Kufuatia kukamilika kwa majadiliano hayo, inasubiriwa kukamilika kwa taratibu za ndani za kisheria kwa kila nchi kuwezesha mkataba kuridhiwa na kusainiwa ili kuanza kutekelezwa.

Majadiliano hayo yameshuhudiwa na Balozi wa Iran nchini Tanzania, Hossein Alvandi Behine na Mkurugenzi wa Idara ya Nchi za Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Abdallah Kilima.

Aidha wajumbe wa pande zote mbili wamezipongeza timu za wataalam kutoka nchi hizo kwa kuendesha majadiliano hayo kwa weledi na kuzingatia maslahi ya kila nchi na hatimaye kuweza kufikia maridhiano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles