29.3 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

Taasisi nne za umma zafutwa, NIDA, RITA zaunganishwa

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, ametangaza kuzifuta taasisi za umma nne na kuziunganisha taasisi  16 ambapo Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA )na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini  (RITA) zimeunganishwa pamoja.

 Mashirika na taasisi za umma zinazofutwa ni Shirika la Uzalishaji la Jeshi la Polisi (TPFCS),Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC), Shirika la Elimu Kibaha (KEC) limenjwa na kuunda Shule ya Sekondari Kibaha au jina litakaloamuliwa na mamlaka na Chuo Cha Ufundi. 

 Bodi ya Pareto imefutwa na shughuli zake kuhamishiwa  katika Mamlaka ya Usimamizi wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA).

 Akizungumza na waandishi wa Habari leo Desemba 15,2023 Jijini Dar es Salaam, Profesa  Mkumbo,  ametaja mashirika mengine yaliyounganishwa kuwa ni Benki ya Kilimo Tanzania (TADB)na Mfuko wa Pembejeo za Kilimo (AGITF) zitakuwa taasisi moja itakayohusika na mikopo na ugharamiaji wa maendeleo ya kilimo nchini.

Bodi ya Chai inaunganishwa na kiwa bodi Moja na Wakala wa Maendeleo ya Wakulima Wadogo wa Chai Tanzania (TSHDA), Bodi ya Nyama na Bodi ya Maziwa zimeunganishwa kuwa taasisi.

Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CARMARTEC), Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) zinaunganishwa pamoja.

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Mamlaka ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) zinaunda i taasisi moja itakayoratibu uwekezaji wasekta binafsi wa ndani na kutoka nje ya nchi.

Taasisi ya Utafiti wa Chai Tanzania (TRIT), Taasisi ya Utafiti wa Tumbaku Tanzania (TORITA) na Taasisi ya Utafiti wa Kahawa (TACRI) zinaunganishwa na kuwa sehemu ya muundo wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI).

Profesa Mkumbo amesema lengo  la kufanya hivyo ni kuimarisha utendaji wa mashirika ya umma ili yaweze kutoa mchango katika maendeleo ya Taifa.

 Amesema kutokana hotuba ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan aliyoitoa bungeni April 22,  2022 alielekeza kufanya mapitio na uchambuzi wa kina kwa mashirika ya umma ili yaweze kujiendesha kwa faida.

Alieleza kuwa Serikali iliunda timu ya wataalam kwa ajili ya kufanya uchambuzi wa kina kuhusu utendaji wa mashirika hayo kwa lengo la kubainisha changamoto za kiutendaji na kupendekeza hatua za kuchukua katika kuongeza tija ya maendeleo nchini.

“Katika awamu ya kwanza serikali umeridhia na kuelekeza kuunganishwa kwa mashirika na taasisi 16 na kufuta mashirika na taasisi nne.

“Kwa uamuzi huu hospitali ya Tumbi Kibaha haitakuwa tena sehemu ya Shirika la Elimu Kibaha bali hospitali ya Mkoa wa Pwani na Msajili wa Hazina ameshaelekezwa kukamilisha taratibu husika za makabidhiano na Wizara ya Afya,”amesema Profesa Mkumbo. 

Aidha Profesa Mkumbo amewatoa wasisi watumishi wote wa umma walio kwenye taasisi hizo kuwa hakuna mtumishi atakaye poteza ajira yake, maslahi yao yote yatalindwa na kuzingatiwa kwa kufuata sheria na kanuni za utumishi wa umma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles