Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Mwenyekiti wa Umoja wa anawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda ameongoza na kundi la wanawake wa Jumuiya hiyo kwenda kukabidhi zawadi kwa mama aliyejifungua mara baada ya kutolewa kwenye tope.
Akizungumza leo Desemba 7, mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo Mwenyekiti Chatanda amesema UWT imeamua kurudi tena kuja kukabidhi nguo za mama na mtoto mchanga pamoja na za mabinti wawili wa mama huyo ambao ni wahanga mara baada ya kuona kuwa anauhitaji wa haraka hili kuweza kumsitiri yeye na watoto wake.
“Leo tumekuja na magodoro, blanketi, shuka, nguo za mtoto, nguo za mama, nguo za watoto wa kike waliookolewa, mabeseni, fedha taslimu Sh 620,000 pamoja na mahitaji mengine ambayo yatamsaidia kuanzia maisha kwa sasa,“amesema Chatanda.
Aidha, katika msafara huo wa Mwenyekiti Chatanda ameongozana na Wadau wa Maendeleo akiwemo Husein Gonga ambae ametoa Bati 50 kwa ajili ya mama huyo ajengewe nyumba na ahadi mbali mbali kutoka kwa wabunge wanawake walioambatana naye.