27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wasira akubaliwa kumkatia rufaa Bulaya

Untitled-1Na Judith Nyange, Mwanza.

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mwanza imekubali maombi  yaliyowasilishwa na wapiga kura wanne wa  Bunda Mjini dhidi ya Mbunge wa Jimbo hilo, Ester Bulaya, Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Wapiga kura hao kupitia kwa mawakili wao, Costantine Mutalemwa na Yasin Memba,    waliiomba mahakama  kuwaongezea muda wa kuwasilisha maombi yao   baada ya muda wao wa awali wa siku 14 kupita.

Pia waliomba  ruhusa ya kuwasilisha  rufaa katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania.

Akitoa uamuzi huo jana, Jaji Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Joaquine De-Mello, alisema mahakama hiyo imekubaliana na maombi yaliyowasilishwa na wapiga kura hao ya kuomba  kuongezewa muda.

Pia ilikubaliana maombi ya  kibali cha kuwasilisha  maombi ya rufaa katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania dhidi ya uamuzi wa shauri namba moja la mwaka 2015 la kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Bunda Mjini uliotolewa na Jaji wa Mahakama hiyo, Mohameid  Gwae.

“Mahakama imekubali maombi namba 38 ya mwaka 2016 yaliyowasilishwa na wapiga kura wanne wa Jimbo la Bunda kupitia kwa mawakili wao Yasin Memba na Costantine Mutalewa.

“Baada ya kupitia hoja za zote ziliozotolewa na mawakili pamoja na uamuzi wa Mahakama ya Rufaa ya  Tanzania katika kesi ya Gobless Lema  kuhusu haki ya mpiga kura kufungua shauri mahakamani.

“Mahakama imebaini kuwa tafsiri ya haki ya wapiga kura iliyotolewa na katika kesi ya  Lema na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania tafsiri yake haipo wazi hivyo imewaruhusu  kuwasilisha maombi yao ya  rufaa dhidi ya uamuzi uliotolewa na Jaji Gwae  mahakama hiyo iweze kutoa tafsiri sahihi kuhusu haki ya mpiga kura,” alisema Jaji De-mello.

Akizungumza nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza baada ya uamuzi huo kutolewa, Wakili wa wapiga kura hao, Yasin Memba, alisema amefurahishwa na uamuzi huo wa mahakama na anakwenda kuandaa maombi  ya rufaa  aweze kuyawasilisha katika Mahakama ya  Rufaa ya Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles