25.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 6, 2024

Contact us: [email protected]

TAMWA yahimizwa kuweka mkazo ajenda ya uhuru wa kujieleza unaojumuisha sauti za wanawake

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Chama cha Waahandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimetakiwa kuweka mkazo katika uhuru wa kujieleza unaojumuisha sauti za wanawake ndani ya ajenda ya jumla ya haki za binadamu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 36 ya chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama wakati alipomuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan katika maadhimisho ya miaka 36 ya Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Waziri Mhagama ametoa wito kwa (TAMWA) kuona umuhimu wa mijadala yenye mlengo wa kijinsia na uhusiano kati ya uhuru wa vyombo vya habari, ulinzi na usalama wa Waandishi wa Habari Wanawake, na uhuru wa kujieleza kuwa kitovu cha kufanya maamuzi katika ngazi ya jamii, kitaifa, na kimataifa.

“Tuadhimishe siku hii kutimiza ahadi zilizotolewa na kila Nchi Mwanachama wa Umoja wa Mataifa ili kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yote na hasa lengo namba tano linalozungumzia usawa wa jinsia,” amesema.

Aidha, wadau mbalimbali wa habari wametumia siku hii kusherehekea kwa kuungana na TAMWA kulinda na kuthamini haki za wanawake, haki za wasichana, haki za watoto, maadili ya kitanzania na kupinga ukatili wa jinsia majumbani, hadharani na mitandaoni.

“Wamiliki wa vyombo vya Habari na waandishi wote kwa ujumla muungane katika jitihada za ulinzi na usalama wa waandishi wa Habari wanawake na hapa niwatie moyo waandishi wa Habari wanawake kuwa kazi yenu nzuri inaonekana pale mnapoweka jitihada ya kufanya kazi kwa weledi bila kukatishwa tamaa na vikwazo vya kimazingira,” amesema Mhagama.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa sasa wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA), Joyce Shebe katika Maadhimisho ya Miaka 36 ya chama hicho.

Amesema kama kauli mbiu inavyosema, Uongozi Bora na Mchango wa Wanawake ni Chachu Kuelekea Tanzania yenye Maendeleo endelevu.

“Hatuna budi kutambua kwamba suala la jinsia siyo suala la wanawake peke yao bali ni suala la kuchochea maendeleo ya taifa letu miongoni mwa wanawake na wanaume, kwani ni jambo linalohimiza ushirikishwaji na ujumuishi usioacha kundi lolote nyuma.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Technolojia ya Habari, Selestine Gervas Kakele amesema inatambua mchango wa TAMWA na wakati wote Serikali itaendelea kuangalia ujumbe ambao TAMWA na asasi nyingine inatoa.

“Tumepokea utafiti kuhusu unyanyasaji wa kijinsia: TAMWA kupitia utafiti huu imesaidia kuvunja ukimya, matokeo ya utafiti hayalengi kunyoosha kidole kwa mtu, bali kushirikiana ili tuweze kuishinda vita hiyo.

“Tusimamie weledi na nidhamu ya kazi na pale vitendo hivi vinapojitokeza: wahanga wasikae kimya jitokezeni, pazeni sauti na serikali itasikia,” amesema.

Awali, Mwenyekiti wa TAMWA, Joyce Shebe amemshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali mwaliko.

“Tumeona jinsi Serikali ambavyo inapitia mifumo ya kisera na kisheria ilikuja na mipango inayopimika katika kuhakikisha ushirikishwaji na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi na masuala yanayohusu usawa wa kijinsia inatatekelezeka,” amesema Shebe nakuongeza kuwa:

“TAMWA tunaahidi kumuunga mkono kivitendo kwa sababu ni jukumu ambalo tumealianza tangu miaka 36 iliyopita,” amesema Shebe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles