25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

ITA yatakiwa  kutafuta suluhu ya ukwepaji kodi

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Chuo Cha Kodi (ITA) nchini kimetakiwa  kufanya utafiti wa kutatua changamoto za forodha na kodi ili kupata suluhu ya ukwepaji kodi  na kubuni vyanzo vipya vya ulipaji.

Agizo hilo limetolewa  na Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande leo Novemba 24,2023  kwenye mahafali ya 16 ya Chuo cha Kodi, jijini Dar es Salaam.

Chande  serikali inawategemea wahitimu hao kutatua  changamoto  mbalimbali na kuboresha mfumo wa kodi na forodha.

“Katika utafiti  utakaofanywa  uende kutatua changamoto za forodha nakodi na kuleta suluhu ili watu walipe kodi kwa hiyari  na kodi stahiki iwe inakusanywa kwa wakati, “amesema.

Amesema Mamlaka ya Mapato nchini (TRA)  inawajibu wa kusaidia kupanua wigo kwa wadau wengi ili serikali ipate wataalamu  wa katika eneo hilo.

 Chande amesema walipa kodi wengi  elimu yao ni ndogo, wamebaini changamoto hiyo, hivyo Chuo cha Kodi  kianzishe kozi fupi kwa ajili ya walipakodi

” Washauri wengi wa walipakodi wana taaluma ya upande  mmoja, inabidi wawe na taaluma ya kodi na uhasibu ili waweze  kuwa washauri wazuri katika  masuala ya kodi,”amesema.

Aidha amewataka wahitimu kutokana na taaluma zao,  wakaanzishe kampuni na kuwa mabalozi wazuri wa chuo  hicho  kwa kufanya kazi kwa waledi.

Amewaomba wahitimu hao  kuwa wanakwenda  mtaani  na huko kuna mambo mengi wakafanye mambo ambayo yanaendana na maadili  ya kitanzania.

Naye Kamishina Mkuu  wa TRA , Alphayo Kidata, amesema  wakaendeleze elimu  waliyopata kuleta  maendeleo  kwa jamii.

“Yale mliyosomea  na mambo ya  kodi mkafanye kazi kwa waledi na mkalete maendeleo ya  Taifa  na kukuza  uchumi  kupitia elimu zenu,”amesema Kidata.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Isaya Jairo, amesema  chuo ni mhimili wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) katika kukidhi mahitaji  ya mafunzo  kwa watumishi wake kwa asilimia 70.

“Kila mwaka  wafanyakazi wa mamlaka hiyo  wanapata mafunzo katika chuo cha kodi, katika  mwaka  wa masomo wa 2022/23 jumla ya wahitimu 508 wamefuzu masomo  yao na wanatarajia kutunukiwa vyeti katika ngazi mbalimbali, “amesema Profesa Jairo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles