22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

St Mary’s yatoa siri ufaulu wa juu

Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Shule ya Msingi, St. Mary’s Tabata, Thomas Samson, amesema kuwa siri ya mafanikio ya shule hizo ni kuwa na walimu bora wanaotambua wajibu wao na kufanyakazi usiku na mchana kuhakikisha wanafunzi wanaelewa.

Ametoa kauli hiyo jana baada  kutangazwa kwa matokeo ya darasa la saba Kitaifa  kutokana  na wanafunzi wake wengi kupata wastani wa alama A kwenye matokeo yao.

Katika matokeo yaliyotangazwa jana  Novemba 23,2023 na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), wanafunzi wengi wa shule hizo wamefaulu kwa alama A, huku wachache wakifaulu kwa wastani wa B.

Amesema walimu wa shule hiyo wamefanyakazi kubwa ya kuwaandaa wanafunzi wake kwa kuwapa mitihani ya majaribio ya mara kwa mara hivyo wanafunzi wake kufaulu mitihani ya darsa la saba haijawashangaza.

 Amesema walianza kuona dalili nzuri ya kufaulu kwa wanafunzi baada ya kuwa wanafanya vizuri zaidi kwenye mitihani ya majaribio ya kimkoa na  kiwilaya ambapo nako walikuwa wanapata wastani wa alama A.

“Sisi tunachojua ni kufundisha, mzazi ukitukabidhi mtoto wako ukae ukijua kwamba umemleta sehemu sahihi, hata kama alikuwa chini tutamfundisha mpaka atakwenda na kasi ya wenzake wenye matokeo mazuri,”amesema Samson.

 Naye Mkuu wa Shule ya Msingi St Mary’s Mbezi, Isaac Tamaro, amesema amefurahi kuona wanafunzi wake wamefaulu kwa kiwango cha juu na kuahidi kuwa hawatabweteka na matokeo hayo na badala yake wataongeza juhudi.

 “Siri ya ufaulu huu ni moja tu kufundisha na kuwawekea wanafunzi mazingira mazuri ya kujifunza kwa kuwapa vitabu vya kutosha na walimu wenye kujua wajibu wao kwamba ni kufundisha tu na kwa kweli matokeo ya juhudi zetu tumeyaona nawapongeza walimu,” amesema Tamaro.

 Amesema wanafunzi  wa shule za St Mary’s wamekuwa wakipewa motisha mbalimbali wanapofanya vizuri ikiwemo kupelekwa kwenye mbuga za wanyama kama Mikumi, Serengeti, Ngorongoro na Ruaha kwa ajili ya kutalii na kujionea wanyama mbalimbali.

 “Tunaushukuru uongozi wa shule za St Mary’s kwa kuendelea kujali walimu wake na kuweka mazingira mazuri ya wanafunzi kusomea, binafsi naona hii imekuwa chachu ya mafanikio haya na tunawashukuru wazazi kwa kutuamini na sisi tunawaahidi kwamba tutaendelea kufanya vizuri zaidi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles