29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Mwambusi: Yanga tulieni muone mambo

mwambutsi-jumaNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

KOCHA msaidizi wa kikosi cha Yanga, Juma Mwambusi, amewatuliza ‘mzuka’ mashabiki na wanachama wa timu hiyo, akiwataka wasubiri waone jinsi wanavyochukua ushindi mfululizo licha ya kubanwa na ratiba.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara, wamekuwa na kipindi kigumu baada ya kukabiliwa na kibarua cha kucheza mechi nne za mashindano matatu tofauti ndani ya siku 10.

Yanga itaanza kushuka dimbani kesho kuwania kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya FA, Jumamosi itaanza harakati ya kumaliza mechi zake za viporo vya Ligi Kuu ambapo itacheza na Kagera Sugar na Aprili 6 ikicheza na Mtibwa Sugar, huku Aprili 9 ikichuana na Al Ahly ya Misri hatua ya 16 bora ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mwambusi alisema wanatambua wanakabiliwa na kipindi kigumu kutokana na ratiba hiyo, lakini watahakikisha wanapata ushindi kwa kila mchezo.

“Tuna kipindi kigumu sana cha kuhakikisha tunacheza mechi zote hizo kulingana na ratiba ilivyopangwa, lakini nawaambia mashabiki wetu watulie na watuunge mkono na waje wajionee jinsi tutakavyochukua ushindi kwa kila mchezo, tunaweza tusiwaonyeshe soka kama la Barcelona lakini tukawaridhisha kwa matokeo.

“Tutaanza kuchukua ushindi kwa Ndanda na tutafuatia na mechi zetu za Ligi Kuu na kuwafunga Waarabu kama tulivyofanya kwa timu nyingine tulizocheza nazo kwenye michuano hii ya kimataifa,” alisema.

Alisema kikosi chao kinakabiliwa na wachezaji wengi majeruhi, lakini watajitahidi kuwatumia walio wazima  kufanikisha mpango wao wa kupata ushindi.

“Baadhi ya wachezaji wetu ni majeruhi na miongoni mwao wapo waliokuwa na majeruhi ya muda mrefu, lakini tutajitahidi kuwabadilisha hawa waliofiti ili kuisaidia timu kufikia malengo wakati wengine hali za majeruhi zikiendelea kuimarika,” alisema.

Aliwataja wachezaji hao kuwa ni Kelvin Yondani ambaye alipata majeraha akiwa na timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Mbuyu Twite, Donald Ngoma, Said Makapu, Malimi Busungu, Geofrey Mwashiuya na Deus Kaseke.

“Kwa mujibu wa daktari wa timu, Yondani bado analalamika kupata maumivu kwenye mbavu, Ngoma anaendelea kuifuatilia hali yake kama anaweza akacheza kwenye michezo ijayo sambamba na hao wengine,” alisema.

Mwambusi alisema Yanga bado wana kikosi kizuri ambacho kinaweza kuwapa matokeo ya kuridhisha na ndio maana wanazidi kupata uhakika wa kufanya vizuri kwenye mashindano yote wanayoshiriki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles