27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Nchi jirani ruksa kutumia Reli za Tanzania-Serikali

Na Mwandishi wetu, Mtanzania Digital

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara amesema kufutia mabadiliko ya Sheria katika Mashirika ya Reli hapa nchini hivi sasa kampuni binafsi na mashirika ya reli katika nchi jirani zitapata fursa ya kutumia Reli kusafirisha mizigo yao kupitia Tanzania na sehemu nyingine.

Akizungumza Septemba 27, 2023 jijini Dar es Salaam katika kikao cha Ushoroba wa kati kilichohudhuriwa na Makatibu Wakuu wa Uchukuzi kutoka Rwanda, Uganda, Burundi, Malawi, Zambia, Tanzania na DRC, Prof. Kahyarara ameomba nchi hizo kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha miundombinu na kutumia Sekta ya Uchukuzi kama nguzo ya Maendeleo ya Kiuchumi badala ya huduma.

“Hatua kubwa zinazochukuliwa na Serikali ya Mheshimiwa Rais Dk. Samia Samia Suluhu Hassan ni Kuanzisha Usafiri wa kubeba mabehewa kupitia Ziwa Viktoria na Tanganyika,” alisema Prof. Kahyarara.

Kahyarara amesema tayari meli ya kubeba mabehewa kutoka Bandari ya Mwanza kwenda Port Bell Uganda imekamilika na wakati wowote itaanza kazi.

“Meli hii itabeba mabehewa ishilini na mbili na inafursa kubwa kuwezesha nchi hasa za Uganda, Sudan ya Kusini na nchi nyingine kutumia reli zao,” ameongezea Prof. Kahyarara.

Kwa upande wake katibu mkuu wa uchukuzi toka Burund, Chrisine Niragira ameimiza matumizi ya reli kwa nchi wananchama ,amesema wakitumia Reli kusafirisha Mizigo itasaidia kuokoa Barabara zisiharibike na kutumika kwa muda mrefu.

“Reli inabeba Mzigo mkubwa hivyo nchi wanchama ni muhimu kutumia reli kwani inasaidia kupunguza gharama na pia itasaidia kulinda Barabara zetu amabazo zinajengwa kwa gharama kubwa,’’ amesema Niragira.

Katika mkutano huo Malawi na Zambia wamejuinga katika Ushoroba huu hivyo kupitia ushoroba huo changamoto nyingi zitazungumzwa na kutafutiwa ufumbuzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles