27.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

EWURA yavipiga Stop vituo viwili vya mafuta Tabora na Morogoro

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Mamlaka ya  Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA ) imefungia utoaji wa huduma ya mafuta kwa  muda wa miezi sita kwa vituo viwili ambavyo ni Camel Oil cha Msamvu na Mtemba Tuliani vyote vya Morogoro kwa tuhuma za kuficha mafuta.

Wakati huo huo EWURA imefungia kwa muda usiojulikana kituo cha Ipuli Tabora mjini kwa muda  usiojulikana cha Kampuni ya GBP huku ikiitaka kampuni  hiyo kujieleza ni kwanini wasiwafungie vituo vyote.

Akizumgumza leo Septemba 4, jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dk. James Mwainyekule amesema baadhi ya  wafanyabiashara wamekuwa siyo waaminifu kwa wanahodhi mafuta bila kujali nchi yao na kwamba wanafanya kinyume cha sheria na utaratibu.

Amesema wafanyabiashara lazima watii sheria, miongozo na utaratibu watambue kuwa vyombo vya Serikali vipo kazini na hawana lengo la kuwatisha wadau.

“Hii biashara inaendeshwa kwa sheria na kanuni na hii  biashara sio holela EWURA tuna utaratibu hivyo kuna  baadhi ya kampuni tumezifungia kwa muda wajitafakari jinsi ya kufanya biashara hii kama sheria inavyotaka,”amesema Dk. Mwainyekule.

Ameongeza kuwa wafanyabiashara wamekuwa  wakichukua mafuta na kuchelewesha kufika vituoni wengine wakiwa na mafuta kwenye visima lakini  hawauzi.

Ameeleza kuwa kupungua kwa dola ni mfumo wa soko  la dunia changamoto ya kuagiza mafuta kwa dola kwa sababu wafanyabiashara nchini wanauza kwa shilingi.

Akizumgumza kuhusu hali ya mafuta nchini Dk. Mwainyekule amesema nchini kuna mafuta ya kutosha kuna mafuta mengi kwenye maghala na mengine yapo kwenye meli zilizowasili bandarini zipo kwenye foleni ya kushusha ambayo yanakidhi mahitaji ya siku 19.

Amesema pamoja na mafuta hayo meli zitaendelea kuwasili hadi Oktoba 31, mwaka huu kulingana na mpangilio ulianishwa katika zabuni za uagizaji mafuta kwa pamoja (BPS) zilizofanyika Agosti 31, mwaka huu.

Amesema wanaendelea kufanyia uchunguzi vituo  vingine 10 juu ya utetezi utakaowakilishwa na vikibainika kukiuka mashariti ya leseni watachukuliwa hatua ikiwemo kufungiwa miezi sita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles