25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

FCS: Teknolojia ni chachu ya kukuza maenedeleo nchini

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mkurugenzi wa Foundation For Civil Society (FCS), Francis Kiwanga, amesema Teknolojia inaweza kuwa chachu ya kuongeza kasi ya maendeleo pamoja na kuwawezesha Watanzania kuongeza uzalishaji, kutafuta masoko na hatimaye kukuza vipato vyao.

Kiwanga ameyasema hayo wakati wa uzinduzi rasmi wa Wiki ya Azaki uliofanyika Agosti 1, 2023 jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society (FCS), Francis Kiwanga, (wa pili kushoto), akiwa na Mbunge wa Kigamboni Dkt. Faustini Ndugulile pamoja na wadau wengine wakipiga makofi mara baada ya kufanyika kwa uzinduzi rasmi wa Wiki ya Azaki iliyozinduliwa Agosti 1,2023 jijini Dar es Salaam.

Amesema lengo la kuwepo kwa Wiki ya Azaki ni kutazama kwa jinsi gani maendeleo ya teknolojia yanavyoweza kuwawezesha Watanzania kuongeza uzalishaji, kutafuta masoko na hatimaye kukuza vipato vyao.

Aidha, ameeleza kuwa mwaka 2018 Wiki ya Azaki ilifanyika kwa mara ya kwanza ambapo pamoja na mambo mengine walijifunza namna ya kuimarisha uhusiano na Serikali.

“Mnamo mwaka 2018 tulikutana kwa mara ya kwanza kwa ajili ya CSO Week, tulianza kujiuliza tunawezaje kuimarisha mahusiano yetu na Serikali.

“Lengo jingine lilikuwa ni kuwajengea uwezo (Capacity Building) kwa wananchi wa kawaida, ili kuweza kuboresha maisha yao, na kuleta tija katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo wananzozifanya” amesema Kiwanga.

Pia ameongeza kuwa, kufanyika kwa Wiki ya Azaki mwaka huu kutakuwa ni mwendelezo ikiwa ni mara ya tano kuzindua ikiwa ni kuelekea kwenye Wiki ya Azaki itakayofanyika Oktoba, mwaka huu, lengo likiwa ni kuwagusa wananchi wanaowapa nguvu ya kufanyakazi kila siku.

“Binafsi kwa mfano, ninapata nguvu ya kufanya kazi kila ninapoona picha ya mama mmoja toka kijijini, akiwa na furaha na tabasamu kubwa baada ya kupata mavuno yake, hawa ndio wanaotupa msukumo wa kuendelea kufanya kazi na kufanya CSO Week kila mwaka,” amesema Kiwanga.

Mkurugenzi Mtendaji wa (FCS), Francis Kiwanga, (wanne kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndugulile (wa tano kushoto) na wadau wengine katika hafla hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Wakili Anna Henga, amebainisha kuwa moja ya haki za msingi za binadamu ni kufikia huduma za teknolojia ambapo amesema ukuaji wa Sayansi na Teknolojia utawezesha wananchi kupata taarifa mbalimbali kuhusiana na haki zao kupitia vifaa vya teknolojia.

“Wiki ya Azaki inaleta pamoja Asasi za Kiraia ( AZAKI) Pamoja kutoka Tanzania nzima kwa ajili ya tukio la wiki moja lenye lengo la kujadili na kuboresha ushirikiano wa kimkakati ikiwa na Kauli mbiu isemayo ‘Teknologia na Jamii, tulipotoka, tulipo sasa na tunapoelekea, kuangazia fursa na changamoto zinazotokana na ulimwengu wa teknolojia unaoendelea,” amesema Wakili Henga.

Mratibu wa Wiki ya AZAKi 2023, Justice Rutenge akizungumza katika hafla hiyo kuelezea namna kaulimbiu ya mwaka huu ilivyobeba dhima nzima ya Wiki ya Azaki.

Mratibu wa Wiki ya AZAKi 2023, Justice Rutenge ameelezea kuhusu uchaguzi wa kaulimbiu ya mwaka huu iliyobeba dhima nzima ya Wiki ya Azaki ambapo amesema ulifanywa kwa madhumuni na inalenga kuziwezesha asasi za kiraia kufahamu na kupata utaalamu unaohitajika ili kuishauri Serikali na sekta binafsi juu ya faida na vikwazo vinavyotokana na teknolojia kwa maendeleo ya nchi.

Wiki ya Azaki inatajiwa kuanza rasmiOktoba 23, hadi 27, mwaka huu jijini Arusha, ambayo inatokana na mafanikio ya matoleo yake ya awali ya mwaka 2018, 2019, 2021 na 2022, ambapo kwa mwaka huu inatarajiwa kuwa chachu ya mabadiliko, kukuza uelewa wa kina wa athari za teknolojia kwa jamii na nafasi yake inayowezekana katika kuunda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles