25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi wasusia mkutano wa Lissu Geita

Na Mwandishi Wetu, Geita

Mambo yameonekana kuwa magumu kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Tundu Lissu baada ya kuahirisha mkutano wake kutokana na kukosa watu katika Kijiji cha Ilolangula, wilayani Mbogwe mkoani Geita.

Mkutano wa Lissu ulipangwa kufanyika leo Agosti mosi, 2023 saa sita mchana katika Kijiji hicho kama sehemu ya mwendelezo wa ajenda ya mikutano yao inayofanyika Kanda ya Ziwa.

Lissu aliingia kijijini hapo na timu yake kwa ajili ya mkutano huo, hata hivyo aliamua kuahirisha kuendelea na mkutano huo kama njia ya kuepuka mfululizo wa kutopata watu wa kutosha kama alivyotarajia.

Chadema wamezindua ziara za mikoani wakianzia na mikoa ya Kanda ya Ziwa, ambayo hata hivyo imekuwa ikipitia changamoto ya kukosa wahudhuriaji ikilinganishwa jna ile ya Chama Cha Mapinduzi.

Hta hivyo inaelezwa kuwa chanzo cha hali hiyo kinaelezwa kuwa ni wananchi kuchukizwa na mwenendo wa Lissu kutoa lugha ya kuudhi anapokuwa anatoa hotuba yake.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Lissu alifika mbali baada ya kuamua kutumia muda mwingi kuwakashifu viongozi wa Serikali, akiwemo Hayati Benjamin Mkapa kwa kumuita mwizi wakati wa utawala wake na kuzalisha chuki dhidi ya wananchi wastaraabu nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles