25.6 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia: Tunachekwa na majirani kwa kuvutana kwetu kuhusu Bandari

*Prof. Mbarawa awekezaji ukikamilika utachangia asilimia 67 ya bajeti

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ameweka msimamo wa uwekezaji wa Bandari kupitia Kampuni ya DP World, akisema malumbano hayawezi kupewa nafasi kwenye mkakati wa kiuchumi.

Rais wa Samia ameyasema hayo leo Ijumaa Julai 14, 2023 wakati wa kuwaapisha Viongozi wateule hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mwendelezo wa Serikali kutoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya watu wanaotumia muda mwingi kurumbana, hali inayochelewesha uwekezaji huo na kutoa mwanya kwa majirani zao kuweka nia ya kupita njia wanayopitia.

“Ndugu zangu wakati sisi tunalumbana kuhusu huu uwekezaji, wenzetu tumeona nao wakionesha njia ya kutafuta mtu wa kuwekeza kwenye bandari yao,” amesema Rais Samia.

Mara baada ya Serikali kutangaza mpango wa kuwekeza kwenye bandari ya Dar es Salaam, baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wamekuwa wakipinga, hali iliyomuibua Rais Samia kutoa ufafanuzi.

Mapema leo Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akizungumza kakao na Wahariri na waandishi wa Vyombo vya habari nchini amesema kuwa karibu dunia nzima kampuni binafsi ndizo zinaendesha bandari.

“Ukiangalia kuna kampuni 10 dunia ikiwamo DP World ambazo ndizo zinaendesha bandari mbalimbali, hivyo niwasihi Watanzania kwamba tuko katika njia sahihi na hii itaenda kubadilisha kabisa uchumi wa Taifa letu.

“Tunahitaji kuwatea maendeleo wananchi wetu, kama tutaweza kupata mwekezaji na kusimamia vizuri bandari yetu basi asilimia 67 ya bajeti yetu yatatoka bandarini,”  amesema Profesa Mbarawa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles