Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital
Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) umeeleza kuwa wanaendelea na mirada ya ujenzi wa nyumba za umma katika mikoa mbalimbali ikiwemo Arusha.
Akizungumza Julai 11, jijini Dar es Salaam, Mtendaji Mkuu wa TBA, Arch. Daudi Kondoro alipotembelea Banda la wakala hao lilipo kwenye maonyesho ya 47 ya biashara amesema miradi hiyo inatekeleza kwa fedha za ruzuku hivyo wanalazimika kuikamilisha kwa wakati.
Amesema licha ya kutumia pesa za ruzuku katika kutekeleza miradi pia wanatumia pesa za makusanyo ya kodi za pango katika kukamilisha miradi hiyo.
“Wakala unafanya kazi kubwa sana katika kutoa elimu na kuonyesha miradi inayofanya ili kutoa fursa Kwa umma kujua shughuli zinafanywa na TBA,” amesema Arch. Kondoro
Amesema wakala ulikuwa unatekeleza ujenzi wa miradi ya umma lakini sasa wanatarajia kuanza kufanya kazi na sekta binafsi ikiwa ni kutekeleza kauli ya Rais Dk. Samia Suluhu aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa nyumba za magomeni mradi uliotekelezwa na TBA .
Aidha amesema katika maonyesho hayo walitumia kuonyesha Watanzania na wageni miradi waliyonayo na ambayo wameshaitekeleza lakini pia wametoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na TBA katika kutekeleza majukumu yao.