26.5 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Shule ya Sekondari Kamene yaishauri Serikali

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mwalimu Mkuu wa Sekondari Kamene iliyopo Tabata- Kimanga, Ilala, jijini Dar es Salaam, Ally Nyambi ameishauri Serikali kuzishirikisha shule binafsi zinapotokea fursa mbalimbali akitaja mradi mkubwa wa Covid-19 ili manufaa yanayopatikana yasambae kwa Watanzania wengi zaidi.

Mradi huo ulinufaisha shule za sekondari za umma nchi nzima ambapo maelfu ya madarasa yalijengwa huku madawati pia yakinunuliwa kwa kila shule nufaika, ulifanyika mwaka jana.

Akizungumza leo shuleni hapo na Waandishi wa habari, Nyambi alisema fedha za Covid -19 ambazo serikali ilipokea kutoka kwa wafadhili ni vema pia shule binafisi zingefaidika kwani zinasomesha Watanzania wengi kama ambavyo shule za umma zinafanya.

“Ni ushauri wangu tu kwamba wakati mwingine inapotokea fursa kama hiyo basi na sisi wa sekta binafsi tufaidike kwani tunafundisha watanzania wale wale,” anasema Msomi huyo.

Kuhusu masuala mengine yahusuyo sekta ya elimu anasema wamekuwa wakishirikiana vizuri sana katika kuhakikisha vijana wa Kitanzania wanapata elimu bora na hivyo kusaidia ukuaji wa sekta ya elimu hapa nchini.

“Tunaipongeza serikali kwani imekuwa ikitushirikisha kwenye mambo mengi yahusuyo sekta  ya elimu kwani inatambua umuhimu wa mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya elimu nchini,” amesema.

Alisema shule yake ni shule kongwe kwa eneo la Tabata na Ilala kwa ujumla na imekuwa kimbilio la wakazi wa Tabata na maeneo mengine ya Jiji.

“Shule yetu inatoa elimu kuanzia ngazi ya awali(vidudu)  hadi kidato cha Sita na ada zetu ni nafuu sana, mfano kidato cha Sita ada ni shilingi laki tano tu kwa mwaka wakati kidato cha Kwanza hadi cha Nne ada ni shilingi laki nne tu kwa mwaka, tunafanya hivyo ili kuwapa fursa vijana wengi wa Kitanzania kupata elimu bora,” alisema.

Kuhusu ufanisi wa shule yake alifafanua kuwa shule imekuwa ikifanya vizuri sana katika mitihani mbalimbali ya Kitaifa akitoa mfano matokeo ya kidato cha sita ambayo yamekuwa bora sana kwani vijana karibu wote wamekuwa wakipata ufaulu wa kiwango cha daraja la kwanza.

“Nitoe wito kwa wazani walete vijana wao hapa ili wafaidike  na ubora wa elimu tunayotoa hapa kwa manufaa yao na manufaa ya taifa kwa ujumla kwani hapa tutapata madaktari, waalimu na watanzania ambao watalitumikia taifa katika nyanja mbalimbali.

“Shule pia imetia mkazo katika kukuza vipaji vya kitaaluma na vya michezo kwa vijana ili taifa lije kunufaika na vipaji vya vijana wetu.

“Kwenye michezo tuko vizuri, tunadhamini na kuendeleza vipaji vya vijana wetu ili baadaye waje kuwa mabalozi wazuri wa taifa hili,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles