27.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

APRM yawasihi Watanzania kutoa maoni kuhusu Serikali yao

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Mpango wa Hiari wa Nchi za Umoja wa Afrika Kujipima kwa Vigezo vya Utawala Bora (APRM) umewaomba Watanzania kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni juu ya Serikali yao ili waweze kubaini changamoto mbalimbali zinazojitokeza kwenye jamii ziweze kufanyiwa kazi na Serikali.

Hayo yamebainishwa Julai 8, jijini Dar es Salaam alipotembelea maonyesho ya 47 biashara Kimataifa Sabasaba na Katibu Mtendaji wa APRM, Lamau Mpole ambapo amesema Serikali imejitahidi kutatua kero za wananchi ikiwemo upatikanaji wa huduma za kijamii kama maji, afya, elimu, umeme na miundombinu.

Amesema APRM wamekuwa wakibadilishana uzoefu mara kadhaa na nchi nyingine lengo likiwa kubadilishana uzoefu na kutathimin utendaji wa nchi na nchi.

“Tunajiandaa kutoa ripoti ya pili ya nchi tathimini ya utawala bora ifakapo Novemba, mwaka huu wananchi wajitokeze kwa wingi kutoa maoni ni haki yao kikatiba ili Serikali ifanyie kazi changamoto mbalimbali na serikali kutambua maeneo ambayo yanafanya vizuri na kuweza kuyaendeleza,” amesema Mpole.

Amesema tathimini hizo wanazozifanya mara kwa mara kwa nchi na nchi zinatoa nafasi ya kujifunza mazuri ikiwemo masuala ya siasa, utawala bora, maendeleo ya uchumi na usimamizi wake kufanya tathimini ya nchi zote na kutoa ripoti mbele ya wakuu wa nchi.

Amesema APRM imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, REPOA na watafiti wengine kufanya tafiti na kutoa ripoti.

Aidha, amesema Tanzania ilijiunga mwaka 2004 lakini shughuli zake zilianza rasmi mwaka 2006 ambapo ofisi ya APRM zipo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Afrika Mashariki ikiwa na jukumu la kuratibu masuara ya siasa , maendeleo ya kiuchumi na usimamizi wake pamoja na utawala bora.

Mpole amesema changamoto kubwa hadi sasa wananchi hawana uelewa juu ya chombo hicho wamejipanga kuendelea kutoa elimu kwa watanzania wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles