Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital
KAMPUNI ya simu ya Samsung Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya mawasiliano ya Tigo zimeahidi kuendelea kutoa huduma bora na nafuu za kidigitali kwa Watanzania ili kuwawezesha kutumia huduma hizo katika shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato hivyo kuboresha uchumi wao na taifa kwa ujumla
Akizungumza na Waandishi habari, Julai 6, 2023 kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara (sabasaba) Meneja wa vifaa vya Internet kutoka Tigo, Imelda Richard amesema ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia ulimwenguni Watanzania hawana budi kujikita zaidi katika matumizi ya vifaa vya kisasa ili kurahisisha utendaji wao wa kazi.
Vilevile amesema kwa kutambua umuhimu wa suala hilo kampuni hizo zimekuja na simu zenye gharama nafuu ambazo pia zinaweza kupatikana kwa kiazio cha Sh 70,000 au 90,000 na baadaye kulipia 1,000 ama 1,500 kwa mwaka mzima wakati mteja akiendelea kutumia simu husika.
Kwa upande wake Msimamizi wa Mauzo wa Samsung Tanzania, Edwin Byampanju ameeleza kwa simu zinazohusika na ofa hiyo kwa ni Samsung A 04 inayopatikana kwa kuanzio cha 70,000 na A 04s inayopatikana kwa kianzio cha Sh 90,000
“Samsung tumejipanga kwa kila Mtanzania kuwa na simu bora kwa kulipa kidogo kidogo na ofa hiyo kwa simu zetu ni Samsung A04 inayopatikana kuanzio Sh 70,000 unaondoka na simu uku ukiwa unalipa kidogo kidogo na A04s inayopatikana kwa kianzio cha Sh 90,000,” amesema Byampanju.