29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wizara ya Maliasili na Utalii yaja kidigital

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Wizara ya Maliasili na Utalii imeanzisha mfumo wa QR Code ili kumsaidia mtalii wa ndani na nje ya nchi kupata taarifa za utalii kupitia simu yake popote alipo bila kufika kwenye idara yoyote inayohusika na utalii.

Hayo yamebainishwa Julai 2, 2023 na Kaimu Mkurugenzi wa Utalii wa wizara hiyo, Dk. Thereza Mugobi alipotembea banda la wizara hiyo katika maonyesho ya 47 ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Amesema lengo ni kuhamasisha utalii wa ndani kwa wananchi na wageni kutoka nje ya nchi na kwamba wanataraji kuwa na watalii milioni 5 ifikapo mwaka 2025.

“Tumetoka kwenye mfumo wa zamani wa kutumia vipeperushi kuelezea shughuli zetu kwenye sekta mbalimbali za utalii na kuja na mfumo wa kisasa wa kuscan QR Code na unapata taarifa zote za utalii kwenye kila idara popote utakapokuwa duniani,” amesema Mgobi.

Amesema lengo la kuwepo kwa QR Code ni kutoa elimu ya utalii vivutio hifadhi na mbuga kwa wananchi kwa njia ya kisasa ili kuwawezesha kutambua faida na kujifunza utalii popote wanapokuwa.

Aidha, amesema katika maonyesho hayo wataonyesha filamu ya “Royal Tour ” bure hivyo wametoa fursa kwa ambaye hajaitazama kujitokeza kuiona.

Naye, Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi ya maonyesho ya Wizara hiyo, John Felix amesema wanahamasisha utalii ili wawekezaji wajue fursa zinazopatikana kwenye sekta hiyo.

Amesema uwepo wao kwenye viwanja vya sabasaba ni kuendelea kuhamasisha shughuli za kitalii pia kutoa elimu ya matumizi ya Qr code kwa wananchi ili kuepuka kubeba mzigo wa vipeperushi badara yake wapate taarifa za utalii kupitia simu zao janja za mkononi.

“Njia ya vipeperushi imepitwa na wakati kwani njia hiyo imekuwa siyo salama kiafya pale yanapotokea magonjwa ya mlipuko kama Uviko 19 lakini pia upotevu wa kumbukumbu wa taarifa za kitalii pindi unapopoteza kipeperushi kwa kuliona hilo ndiyo maana hapa ukiingia kwenye haya mabanda yetu kila sehemu kuna Qr code hivyo mtu yeyote anaweza kuscan na kupata taarifa,” amesema Felix.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles