MBUNGE wa Ilemela, Angelina Mabula, amewataka wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo ya jirani wajitokeze katika Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Machi 27 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ili lifanikiwe.
Mabula alisema Tamasha la Pasaka ni la Watanzania wote, lakini mwaka huu wamepata bahati ya kufikiwa na ujumbe wa neno la Mungu ambao utakemea maovu yakiwemo mauaji ya vikongwe na walemavu wa ngozi ‘albino’.
“Binadamu anatakiwa kubaki na heshima yake, kwani hakuna maisha bora ambayo yanatokana na kuwaua na kuwakata viungo wenzao, si ubinadamu kabisa tunatakiwa tumrudie Mungu kwani ndio kimbilio,” alisema Mabula.
Mabula alisema tamasha hilo limebeba ujumbe wa neno la Mungu hivyo ni nafasi kwa wakazi wa Ilemela na maeneo ya jirani na hata mikoa mingine kujitokeza kwa wingi kufanikisha tamasha hilo.