26 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mabigwa wa Mtoko wa Kibingwa wapamba Kariakoo Dabi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

HATMAE ndoto ya washindi 100 wa Mtoko wa Kibingwa Msimu wa 5 ya kushuhudia Dabi ya Kariakoo baina ya Simba na Yanga imetimia baada ya jana kushuhudia wababe hao wa soka nchini wakiminyana katika dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba katika mchezo huo yalifungwa Dakika 2 na Enock Inonga akiunga nisha mpira ulipogiwa na Beki Shomary Kapombe huku bao la pili likifungwa dakika ya 32 na Kibu Denis.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa Dabi hiyo Afisa Habari wa Betika, Juvenalius Rugambwa amesema Kumalizika kwa Mtoko wa Kibingwa Msimu wa 5 tayari umekamilisha idadi ya washindi 400 na kuwakonga nyoyo zao washindi hao kwa kushuhudia mtanange huo mkali.

“Mtoko wa Kibingwa imekuwa sehemu kubwa ya burudani katika shamrashamra ya dabi hiyo kubwa ambapo washindi wamepata walichohaidiwa na kampuni ya betika kwa asilimia 100,” amesema Rugambwa.

Rugambwa ameeleza namna washindi hao walivyopata bata la burudani pale Kidimbwi, chakula cha mchana kutoka kwa Shishi food pamoja na Msafara wenye king’ora hadi uwanjani. 

Hata hivyo amehaidi Mtoko wa Kibingwa msimu ujao utakuwa mkubwa zaidi kuliko misimu iliyopita ili kuwapa fursa watu wengi zaidi kushuhudia Ligi hiyo.

“Kila msimu tutaendelea kuboresha zaidi ili kuwapa fursa idadi kubwa ya Mabingwa na sisi betika tumekuwa mfano mzuri kuonyesha kuwa tukihaidi jambo tunatekeleza na kudhihirisha kuwa Mtoko wa Kibingwa hauna Mbambamba,” amesema Rugambwa.

Nae Mshindi wa Mtoko wa kibingwa Rashid Omary amesema kwa upande wake amesema amefurahi mtoko huo wakibabe kutoka betika pamoja na kichapo kutoka kwa simba na kuwashauri watu waiamini kampuni hiyo kuwa haina mbambamba wakihaidi wanatekeleza .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles