Na Mohammed Ulongo, Mtanzania Digital
Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) imewataka wanawake wajawazito nchini kuacha mara moja kutumia pombe hususan zinazotengenezwa na kampuni hiyo sababu ni hatari.
Angalizo hilo limetolewa Dar es Salaam Machi 24, 2023 na kampuni hiyo wakati wa kuzindua kampeni yake ya ‘Mdogomdogo’ huku ikiwasihi watu wanaotumia pombe kuhakikisha kuwa wanazingatia usalama wao.
Kwa mujibu wa TBL kampeni hiyo inalenga kuelimisha wateja juu ya unywaji mbaya na kuepukana na maafa yatokanayo na unywaji huwo holela.
Mkurugenzi wa Uhusiano na Maendeleo Endelevu wa TBL, Mesiya Mwangoka amesema wanajaribu kuhamasisha wanywaji ikuona pale wanapokuwa wamekunywa pombe nyingi kuweza kutafuta uzaidizi wa kufika nyumbani.
“Katika kampeni hii tunasisitiza kuwa wanawake wajawazito wasitumie kabisa vinywaji vyetu sababu ni hatari kwao na kwa mtoto aliyeko tumboni, hivyo mnywaji wa pombe anapaswa kufuata alama zitakazo mwezesha kuwa salama katika unywaji wake, tumezindua kampeni hii ili kuelimisha jamii kuwa mnywaji anapaswa kuzingatia umri wake kabla ya kunywa, kuzingatia usalama wake kutoendesha chombo cha moto akiwa amelewa pamoja na kuwakataza kabisa wajawazito kutumia pombe,” amesemaMwangoka.
Aidha, Mesiya ameongeza kwa kuwataka watanzania kufuata hatua hizo kwani ni muhimu katika kupunguza hali ya unywaji usiofaa ambao unaweza ukasababisha athari kwa binadamu kwa kutofuata utaratibu unaofaa kwa mnywaji ili kumkinga na majanga mbalimbali.
Kwa upande wake Makamu wa Rais ABlnBev, Andrew Whiting amesema wazo la kampeni limekuja kwa ajili ya kuhamasisha watu kuwa wapole na kunywa kistaarabu popote walipo na kuwa waangalifu pindi wanapotumia bidhaa zao na kuzingatia alama tatu zilizoko kwenye bidhaa.