28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Majaliwa akagua ujenzi SGR Mwanza-Isaka

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa leo Machi 26, 2023 amekagua Mradi wa Ujenzi wa reli ya kisasa SGR Mwanza-Isaka, Kipande cha Tano cha Ujenzi wa reli awamu ya kwanza Dar es Salaam Mwanza.

Kipande hiki cha Mwanza-Isaka kina jumla ya kilometa 341, hadi kukamilika kwake kitagharimu Sh Trilioni 3.062.

Kipande hicho kitakuwa na jumla ya vituo vya abiria 10 na vituo viwili vya mizigo vya Fela na Isaka.

Maendeleo ya ujenzi huo umefikia asilimia 28.03 na ujenzi wa tuta ni asilimia 58.4 sawa na kilometa 136 kati ya kilometa 249 za njia kuu.

Mradi huo umetoa ajira zaidi ya 6,720 na kandarasi ndogo zenye thamani ya shilingi bilioni 80 hadi sasa.

Baada ya kukagua mradi huo Mheshimiwa Majaliwa amesema amefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo huku akitoa wito kwa wananchi wa maeneo hayo kuwa walinzi wa vifaa na mitambo inayotumika katika ujenzi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles