26 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

TFNC yawafikia watu wasioona kwa kuandaa nyenzo zenye ujumbe wa lishe

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania kupitia Ufadhili wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) imewafikia watu wasioona baada ya kuzindua nyenzo zenye ujumbe wa lishe kwa kundi hilo, ambazo zimeandaliwa katika maandishi ya nukta nundu na nyingine kwenye mfumo wa sauti.

Uzinduzi huo umefanyika Machi 21, 2023, katika Ofisi za Taasisi ya Chakula jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa lishe akiwemo Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Sarah Gibson.

Akizungumza na waandishi wa habari kitabu cha ujumbe huo wa lishe kwa jamii ya watu wasioona, kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Esther Nkuba amesema kitabu hicho kinalenga kuelimisha na kuhamasisha jamii ya watu wasioona kuhusu umuhimu wa lishe bora kwa ustawi, ukuaji na maendeleo ya watoto na afya ya watu wa jamii hiyo kwa ujumla.

Nkuba amesema Taasisi imeyafikia makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo wanawake wajawazito, wanaonyonyesha, watoto wadogo na wachanga, vijana balehe, na wazee, huku kundi la wasioona likisahulika, hivyo ujio wa nyenzo hii utawasaidia nao kuweza kufikiwa na elimu ya lishe mabayo Taasisi imekuwa ikiitoa.

Kwa Upande wake mwakilishi mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani Sarah Gibson amesema waliamua kuunganisha nguvu na Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania ili kuweza kuandaliwa kwa nyezo hizo zenye ujumbe wa lishe kwa watu wasioona, mara baada ya kugundua jamii hiyo inakosa fursa ya kupata elimu sahihi kuhusu masuala ya chakula na lishe.

“Watu wenye matatizo ya kuona hawawezi kupata taarifa za lishe kupitia vyombo vya habari vya magazeti, kama vile mabango, vipeperushi na vipeperushi. Kwa hivyo, ilikuwa ni lazima kuendeleza afua zinazofaa na zilizolengwa ili kuwahimiza kufuata tabia na mitindo ya maisha chanya ya lishe,” amesema Gordon.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles