27.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kleyah kuzindua video ya ‘The African Drum’

BMiiOkSNNA FESTO POLEA

MKALI wa wimbo wa ‘Msobe Msobe’, Claire Pamela Kamahoro ‘Kleyah’, amepanga kuzindua video ya wimbo wake mpya wa ‘The African Drum’, Machi 19 jijini Dar es Salaam.

Wimbo huo wa mkali huyo wa Afro pop utazinduliwa katika hoteli ya Hyatt Regency ‘Kilimanjaro’ kwa muziki wa ‘live’ kutoka kwa mwanadada huyo.

Katika wimbo wake wa ‘Msobe Msobe’ unaendelea kufanya vizuri katika vituo mbalimbali vya runinga na redio amemshirikisha mkali wa sauti, mpigaji vyombo vya muziki na mmiliki wa studio ya High Table Sound, Barnaba Elias ‘Barnaba Boy’.

Kutokana na kupenda muziki, Kleyah aliacha kazi UNDP kwa sababu ya kuendeleza muziki wake.

“Naamini muziki wangu wa ‘Msobe Msobe’ pamoja na sauti yangu nzuri unanisaidia kuwa wa pekee katika muziki wangu na umenifikisha na kunitambulisha vema hapa Tanzania,” alieleza Kleyah.

Kabla ya wimbo wa ‘Msobe Msobe’ nyimbo mbili za msanii huyo ukiwemo ‘Lovers Eyes’ na ‘Don’t Sly me’ alizozirekodia nchini Afrika Kusini hazikuteka soko la Afrika Mashariki licha ya kufanya vizuri katika chati za muziki nchini humo.

“Kutokufanya vizuri kwa nyimbo hizo ndiko kumenirudisha  Tanzania nikafanya wimbo wa ‘Msobe Msobe’ ili niweze ku ‘win’ soko la Afrika Mashariki kwa kuwa kutoka kimuziki hapa ni rahisi kuliko ukiwa nchi nyingine za Afrika Mashariki kwa kuwa lugha ya Kiswahili inapendwa sana na sasa nakuja na wimbo wa ‘The African Drum’,” alieleza Kleyah.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles