24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Halotel yaunga mkono kampeni ya uchangiaji damu shuleni Kisutu

Na Imani Nathaniel, Mtanzania Digital

Katika kuunga mkono juhudi za Serikali za kuokoa Maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu, Kampuni ya Simu ya Halotel, leo Machi 6,2023 imeshirikiana na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kisutu na Taasisi ya Mifupa- MOI, kuandaa tukio la uchangiaji damu kwa hiari.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko Halotel Sakina Makabu akikabidhi mahitaji na vifaa mbalimbali ikiwemo Tisheti, chakula, vinywaji na vitafunwa kwa Mkuu wa Shule ya wasichana ya Kisutu, Chiku Mhando kwa ajili ya kutumika wakati wa zoezi la uchangiaji damu lililofanyika leo katika viwanja vya shule ya sekondari ya wasichana ya Kisutu jijini Dar es Salaam ili kuunga juhudi za serikali katika upatikanaji damu kwaajili ya wagonjwa mblimbali kayika hospital ya MOI na Muhimbili. Pamoja nao ni Afisa Kutoka MOI, Joel Mushi (Katikati)) na wanafunzi mablimbali kutoka Shule hiyo.

Katika kuelekea siku ya wanawake duniani, Machi 8 ya kila mwaka, Halotel imeona ni muhimu kusherehekea siku hiyo kwa kuchangia katika Sekta ya Afya kwa Kuunga mkono juhudi za serikali kuboresha sekata hiyo.

Halotel ikishirikiana na MOI, imewezesha utekelezaji wa Kampeni  ya Uchangiaji damu chini ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kisutu kwa kuchangia vifaa mbalimbali ikiwamo nguo, chakula, vinywaji na vitafunwa kwa ajili ya kutumika  katika zoezi hili.

Akizungumza katika zoezi hilo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko Halotel, Sakina Makabu, amesema kuwa, katika kuhakikisha tunaipunguzia Serikali ya Awamu ya Sita mzigo katika changamoto ya kukosekana kwa damu ya kutosha na kuokoa maisha ya wagonjwa katika Taasisi ya MOI na Hospital ya Muhimbili.

“Wajawazito, manusura wa ajali, watoto chini ya miaka mitano wapo katika kundi lenye Uhitaki mkubwa wa damu, hivyo kuwezesha zoezi hili ni ishara ya upendo kwa Watanzania ambao pia ni wateja wake, ambapo zoezi hili linatarajiwa kushirikisha zaidi ya shule 40 ambazo zitaleta wanafunzi zaidi ya 2,000,” alisema Sakina.

Kwa upande wa Afisa Habari wa MOI, Patrick Mvungi, amesema kuwa Taasisi hiyo imefurahishwa kwa mwitikio kutoka Kampuni ya Halotel, kwa kuwezesha Kampeni hii .

“Hii inaonyesha namna Kampuni inavyojali Afya za wananchi, na juhudi zinazofanywa na Serikali katika Kuboresha Sekta ya Afya ambapo hii ni hatua kubwa kwetu kuelekea kuimarisha zaidi uhusiano wetu na Kampuni ya Halotel katika Sekta ya Afya,” amesema Mvungi.

Kwa upande wa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kisutu, Chiku Mhando, ameishukuru Halotel kwa kuwa mdhamini mhimu katika tukio hili, huku akiomba makampuni mengine na Taasisi nyingine kujitokeza kuunga mkono zoezi hilo ili kuongeza kiwango cha damu kwenye benki ya damu.

“Halotel ni Kampuni inayotambua thamani katika Sekta ya Afya Nchini, hivyo Taaisis nyingine tunaziomba zifanye hivyo ili kuweza kusaidia benki ya damu kuwa na akiba,” amesema Mhando.

Aidha, sera ya kampuni ya Halotel siyo tu imejikita kibiashara bali pia kusaidia jamii , kurudisha sehemu ya faida kwa jamii ili kusaidia Serikali katika Kuboresha sekta ya afya na elimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles