30.4 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mwakinyo kupanda ulingoni Aprili 22, Dodoma

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Baada ya kukaa kimya muda mrefu bondia Hassan Mwakinyo sasa atapanda uliongoni Aprili 22 kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma kupigana na bondia kutoka Afrika Kusini.

Pambano hilo limeandaliwa na promota maarfu wa kike nchini, Sophia Mwakagenda wa kampuni ya Lady in Red promotion na lina malengo ya kukusanya taulo za kike 40,000 kwa wanafunzi mbalimbali wa mikoa ya  Nyanda za Juu Kusini, Iringa, Mbeya, Njombe na Ruvuma.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Lady in Red Boxing Promotion, Sophia Mwakagenda , akizungumza wakati wa utambulisho wa pambano la Bondia Hassan Mwakinyo (kulia) ambalo litafanyika Aprili 22,2023 kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua taulo za kike 40,000 kwa wanafunzi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. Mwakinyo atapambana na bondia kutoka Afrika Kusini.

Mwakagenda alisema kuwa wamekwisha anza maazungumzo na bondia wa kupigana na  Mwakinyo na watamtangaza mara baada ya kukamilisha mazungumzo hayo.

Alisema kuwa wanatarajia kuwa na pambano la kusisimua siku hiyo kwani wanatarajia kushirikisha mabondia nyota wa kiume na wa kike.

Alifafanua kuwa mara ya mwisho kwa Mwakinyo kuingia ulingoni ilikuwa Septemba 3 mwaka jana ambapo alipambana na bondia Liam Smith mjini Liverpool na kupoteza kwa TKO katika raundi ya nne.

“Tunatarajia kuwa na pambano kali na la kusisimua siku hiyo. Tunarajia mashabiki wa ngumi za kulipwa  Wabunge na viongozi mbalimbali wa serikali kuhudhuria pambano hilo. Tunawaomba wadhamini wajitokeze ili kufanikisha pambano hili,”alisema Mwakagenda.

Kwa upande wake, Mwakinyo alisema kuwa anatarajia kurejea kwa nguvu zote pamoja na kutoingia ulingoni  kwa miezi zaidi ya mitano. Alisema kuwa amejiandaa vilivyo katika pambano hilo na ataonyesha uwezo wake.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Lady in Red Boxing Promotion, Sophia Mwakagenda (wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na bondia Hassan Mwakinyo (wa pili kushoto) mara baada ya kutangaza pambano lililopangwa kufanyika Aprili 22 kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma kwa ajili ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua taulo za kike 40,000 kwa wanafunzi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. Kulia ni  Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) Yahya Poli na Pendo Njau ambaye ni mwaamuzi wa ngumi za kulipwa. Mwakinyo atapambana na bondia kutoka Afrika Kusini.

“Ni kweli kuwa sijapigana muda mrefu na mengi yamesemwa, sasa narejea kwa nguvu zote na kufuta mawazo yote hasi dhidi yangu. Kwa kifupi sipigani kwa lengo la kuwafurahisha baadhi ya watu.. nafanya hivyo kwa ajili ya kukuza kipaji changu,” alisema Mwakinyo.

Mwakinyo alisema kuwa ameanza maandalizi kwa ajili ya pambano hilo na anawaahidi Watanzania kufanya vyema ikiwa anapigana kwa mara ya kwanza mkoani Dodoma.

Wakati huo huo, Mwakinyo amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake kuendeleza michezo na kuleta hamasa kubwa.

Alisema kuwa uteuzi wa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis  Mwinjuma umeongeza hamasa katika michezo, Sanaa na Utamaduni kwani aiyeteuliwa anafaa na ni mdau mkubwa wa sekta hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles