24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

WCF walipa bilioni 44.61 kwa wanufaika mbalimbali nchini

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Hadi kufikia Juni 30, 2022, Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umelipa mafao yenye thamani ya Sh bilioni 44.61 kwa wanufaika mbalimbali.

Hilo ni ongezeko kubwa kwa kulinganisha na kipindi cha kabla ya kuanza kwa WCF ambapo malipo ya fidia yalikuwa chini ya Sh milioni 200 kwa mwaka.

Katika kipindi cha Julai 2022 hadi Desemba 2022, WCF ililipa mafao ya jumla ya Sh bilioni 6.19 kwa wanufaika 1,004 na hivyo kufanya wanufaika wa mfuko toka kuanzishwa kwake kufikia 10,454 ambao wamelipwa jumla ya Sh Bilioni 49.44.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dk. John Mduma amebainisha hayo wakati wa akielezea utekelezaji wa majukumu ya Mfuko huo katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Machi 2, 2023 Jijini hapa.

Mfuko huo umeendelea kulipa fidia hizo kupambana na umaskini na kufanya malipo endelevu (pensheni) kwa wanufaika ambapo kwa Juni 2022, wanufaika 1,114 walilipwa kiasi cha Sh milioni 231.39 kwa mwezi huo.

Dk. Mduma amesema Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imefanya maboresho kadha wa kadha katika kutelekeza andiko maraafu kwa jina la Blueprint kupitia WCF.

Amesema Serikali iliendelea kuleta unafuu zaidi kwa waajiri kwa kupunguza kiwango cha kodi ya malimbikizo ya madeni ya michango ya nyuma kutoka asilimia kumi (10%) hadi asilimia mbili.

“Ili kuhamasisha waajiri ambao hawajajisajili waweze kujisajili na watekeleze wajibu wao wa kulipa michango kwa ajili ya kulinda wafanyakazi wao dhidi ya majanga yatokanayo na kazi.

“Sanjari na hayo, Serikali kupitia WCF imetekeleza sera ya msamaha wa riba kwa waajiri waliochelewesha michango tangu Mfuko ulipoanza mwaka 2015 hadi Juni 2022 kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara,”amesema Dk. Mduma.

Amesema uamuzi wa kushusha viwango vya uchangiaji kwa sekta binafsi unalenga kumpunguzia mzigo mwajiri ili fedha alizokuwa akitumia kuchangia zielekezwe kwenye maeneo mengine ya uendeshaji wa shughuli zake za uzalishaji.

Aidha amesema Serikali kupitia WCF imetekeleza sera ya kuongeza kima cha chini cha fidia hadi kufikia Sh 275,333 kutoka utaratibu wa awali ambao haukuwa na kima cha chini cha fidia kwa mfanyakazi ambaye hakupata ulemavu wa asilimia 100.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles