29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Dar kuendelea kusotea maji

Dr+marry+naguGRACE SHITUNDU NA ROSEMARY MWAIKUGILE (RCT)

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Maji imesema endapo bwawa la Kidunda mkoani Morogoro halitakamilika tatizo la maji    Dar es Salaam halitakwisha.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati hiyo,  Dk. Mary Nagu   kamati hiyo ilipokutana na viongozi wa Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco) na  Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar  es Salaam (Dawasa).

Dk. Nagu alisema kwa muda mrefu upatikanaji wa maji kwa wakazi  wa Dar es Salaam ni tatizo kubwa hali inayosababisha  watu wengi kuugua magonjwa ya mlipuko kikiwamo kipindupindu.

Alisema bwawa la Kidunda lina umuhimu mkubwa katika kutatua tatizo hilo kwa kuwa kuanzia Agosti na Novemba kunakuwa na ukame kutokana na kukosekana   mvua.

“Leo tunataka kujua kutoka kwa Dawasco na Dawasa kuhusu miradi ya maji imefika wapi hasa uchimbaji wa bwawa la Kidunda ambalo kwa kiasi kikubwa ndiyo suluhisho la tatizo la maji hapa jijini.

Pia tunataka kujua Mradi wa Ruvu Chini na Kisarawe 2 ambao uliasisiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete nao umeishiwa wapi kwani hali ni mbaya.  Kinamama wanabeba ndoo za maji wakiwa wajawazito na wanayafuata mbali,”alisema Dk. Nagu.

Alisema kukosekana kwa maji kunachangia kwa kiasi kikubwa magonjwa ya mlipuko hasa kipindupindu   ikizingatiwa Dar es Salaam ni jiji lenye watu wengi na shughuli nyingi za  biashara na viwanda.

Akielezea kuhusu miradi hiyo, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji,  Isack Kamwelwe alisema kwa sasa Dar es  Salam ina upungufu wa maji lita milioni 150 kwa siku.

Alisema maji yanayopatikana ni lita milioni 300 na zinazohitajika ni lita milioni 450 hali inayofanya tatizo la maji kuendelea kuwa sugu.

Hata hivyo, alisema   serikali ina mkakati wa kuhakikisha miradi yote inakamilika ifikapo   Juni ambako inakadiriwa zitapatikana lita milioni 756 kwa siku ambazo zitakuwa ni zaidi ya asilimia 100.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles