25.9 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali itaendelea kutatua changamoto za elimu-Dc Ngaga

Na Anna Ruhasha Mwanza

Mkuu wa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, Senyi Ngaga amesema Serikali itaendelea kutatua changamoto katika sekta ya elimu kwa kuboresha miundombinu ya kujifunzia na kufundishia.

Mwenyekiti wa wakuu wa Shule Mkoa wa Mwanza TAHOSA akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi ambaye alikuwa mkuu wa wiliya ya Sengerema.

Ngaga ametoa kauli hiyo jana wakati akizungumza katika mkutano Mkuu wa Umoja wa Wakuu wa shule za sekondari za Serikali na Binafsi (TAHOSA) Mkoa wa Mwanza alipokaribishwa kama mgeni rasmi.

Amesema serikali bado inatoa fedha katika kuboresha miundombinu ya elimu nakwamba inatambua kazi nzuri inayofanywa na walimu katika kusimamia elimu na kuhakikisha ufahuru unaongezeka mwaka hadi mwaka.

“Kuna changamoto mmezibainisha hususani kwa shule za serikali, uhaba wa mabweni na Walimu wa Sayansi lakini nyinyi ni mashahidi mmeona serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan fedha za Uviko-19 ujenzi wa vyumba vya madarasa, ajira zimetolewa nyingi za walimu lakini niseme serikali haijalala bado changamoto hizo mlizozisema serikali inaendelea kushugulika nazo,” amesema Ngaga.

Upande wake Mwenyekiti wa umoja wa wa wakuu wa shule za sekondari binafsi na serikali, Deus Lugwala amesema kuwa mbali na changamoto za uhaba wa miundombinu za kujifunzia na kufundishia kwa baadhi ya shule wamesema kuwa umoja huo ulianzishwa kwa lengo la kujengeana uwelewa na kusimamia nidhamu kwa wakuu wa shule hao.

Baadhi ya wakuu wa shule wananchama mkuu wa shule ya sekondari Kilabela, Leornad Manyoni akizunguma kwa niaba ya wenzao amesema kuwa umoja huo umewajenga kiutendaji na kinidhamu katika kusimamia taluma na maadili katika kazi.

Hata hivyo, mkutano mkuu wa pili umeenda sambamba na uchaguzi wa kuwachagua viongozi watakao ongoza kwa miaka mitano ijayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles