26.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 18, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia achangia milioni 40 ujenzi wa kanisa la KKKT Mufindi

Na Raymond Minja, Mafinga

Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasasn ameungana na waumini Dayosisi ya Maandalio ya Kanisa la KKKT Mufindi mkoani Iringa kwa kuchangia Sh milioni 40 katika Harambe ya kumalizia ujenzi wa kanisa hilo akiwakilishwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Daniel Chongolo aliyefanikiwa kukusanya zaidi ya Sh milioni 220.

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo akizungumza kwenye hafla hiyo.

Harambee hiyo iliyofanyika Septemba 25, mwaka huu ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kiserekali pamojaa na wabunge wa ndani na nje ya Mkoa wa Iringa.

Akizungumza kwenye harambee hiyo, Chongolo aliwashushukuru viongozi wa kanisa hilo kwa kumpa heshima ya kufanikisha harambee hiyo kwani wako watu wengi lakini wakaona yeye anaweza kuendesha kazi hiyo.

“Niwashukuru kwa kuniamini na kuona nafaa kuja kuendesha shughuli hii na nimshukuru sana Mhe Rais Samia Suluhu kwa kuniruhusuu kuja hapa na nilipomweleza nae kanipaa salamu zenu nami nitaziwakilisha hapaaa.

“Wakati naondoka niliendaa kuomba ruhusa kwa mhe Rais Samia na kumwambia nimeomba na wana-Mafinga kwenda kufanya harambee na akaniambia niwasalimie na mh Rais amenituma niwape Sh milioni 40, anawapenda sana na anawaomba muendelee kuliombea Taifa lenu la Tanzania,” alisema Chongolo.

Kwa upande wake Mkuu wa Dayosisi hiyo, Dk. Antony Kipangula amemshukuru Katibu Mkuu huyo wa CCM kwa kusaidia kufanikisha harambee hiyo ya kumalizia ujenzi wa kanisa.

Dk. Kipangula alimuomba Chongolo kufikisha shukrani kwa Rais Samia kwa kuwaunga mkono kwenye harambee hiyo kwa kuwapa Sh milioni 40.

“Mh katibu mkuuu tukushukiru sana na tuomba pia utufikishie salamu zetu kwa Mhe Rais kwa kufanikisha harambee hiyo na mchango mkubwa mliotoa tunawashukiru sana na tutazidi kuwaweka magotini pa Mungu ili muendelee kuiongoza nchi yetu kwa hekima na busara,” amesema Dk. Kipangula.

Awali, akisoma risala kabla ya harambee hiyo kuanza Katibu wa ujenzi huo, Hezron Myinga alisema kuwa matarajio ya kanisa hilo ni kukusanya Sh milioni 250,000,000.

Alisema kuwa fedha wanazotarajia kukusanya zitafanya kazi ya kunakshi kuta za ndani na nje, ujenzi wa madhabahu na vyoo vya ndani, kutengeneza na kufunga milango na madirisha pamoja na kulipa fidia kwa baadhi ya wakazi wanao zunguka kanisa hilo ilinkuweza kupata nafasi ya kujenga choo pamoja na nyumba za watumishi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles