26.4 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

NMB yatoa vifaa vya Sh milioni 50 Uhuru Hospital Dodoma

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya  NMB ,Ruth Zaipuna (wapili kushoto)  akimkabidhi Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson (watatu toka kushoto)  vifaa kwa ajili ya hospitali ya Uhuru iliyopo Wilaya Chamwino Mkoani Dodoma, kushoto kabisa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu, George Simbachawene NMB ilikabidhi magodoro,vitanda na vifaa tiba vyenye thamani ya sh milioni 50 kwa ajili ya hospitali hiyo.

Na Mwandshi Wetu, Mtanzania Digital

BENKI ya NMB, imekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Sh. Milioni 50, kwa Hospitali ya Uhuru, iliyopo Chamwino jijini Dodoma, ikiwa ni sehemu ya  Programu ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), ambayo Mwaka 2022 ilitengewa zaidi ya Sh. Bilioni 2 sawa na asilimia moja ya faida ya benki hiyo. 

Makabidhiano hayo yalifanyika wakati wa Tamasha la NMB-Bunge Bonanza, lililofanyika viwanja vya Chinangali Park jijini humo, ambako Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, alimkabidhi Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson Mwansasu, aliyepokea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo, Zaipuna alibainisha kwamba NMB inatambua na kuthamini uwajibikaji wake kwa jamii, na kwamba wanaamini msaada waliokabidhi Uhuru Hospital, vifaa hivyo vitasaidia kuboresha mazingira ya kuhudumia wagonjwa hospitalini hapo.

Zaipuna alivitaja baadhi ya vifaa vilivyotolewa na benki yake na kupokelewa na Dk. Tulia, kuwa ni pamoja na vitanda vya dharura, vitanda vya wagonjwa, vitanda vya kufanyia uchunguzi, jokofu la kugandishia, machela ya kubebea wagonjwa, magodoro, mashine za kupima wagonjwa wa moyo, mashuka na vinginevyo.

Aidha, Zaipuna alisema kwamba ukiondoa msaada huo, benki yake iko mbioni kufanya msimu wa pili wa Mbio za Hisani za NMB Marathon ‘Mwendo wa Upendo,’ lengo likiwa ni kukusanya Sh milioni 600 za kusaidia matibabu ya kinamama wenye changamoto ya Fistula wanaotibiwa Hospitali ya CCBRT, Dar es Salaam.

Zaipuna alitumia nafasi hiyo kumkaribisha Spika Dk. Tulia na Wabunge wote, kujisajili kwa ajili ya ushiriki wa mbio hizo, zitakazoanzia kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, ambako mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ili nao wawe sehemu ya wanaorejesha tabasamu kwa kinamama hao.

Kwa upande wake, Dk. Tulia aliishukuru NMB na kuipongeza sio tu kwa namna inavyosaidiana na Serikali katika kutatua changamoto zinazoikabili Sekta ya Afya na Elimu nchini, bali pia kwa jinsi inavyofanya usaidizi huo kwa muendelezo, kama ilivyofanya mwaka jana iliposaidia elimu na mazingira.

“Mmefanya jambo kubwa sana hapa, mmekabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Sh. Mil. 50, kwa ajili ya eneo la afya. Tunawashukuru sana sana kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha sekta ya afya inakuwa bora nchini.

“Nasema mnaunga mkono juhudi za Serikali kwa sababu, wakati Rais Samia Suluhu Hassan anapambana kuboresha miundombinu ya afya kwenye maeneo mbalimbali, na ninyi mnavyopeleka vifaa, basi mnaipunguzia Serikali mzigo wa kutafuta vifaa hivyo na kusambaza hospitalini.

Spika Dk. Tulia alienda mbali zaidi kwa kuitaka NMB isiishie hapo tu, kwani Rais Samia anajenga zahanati, hospitali na vituo vya afya kote nchini, ambako nako kunahitaji aina hiyo ya usaidizi kutoka kwa wadau wakubwa kama NMB, ambao mchango wao bado unahitajika.

Kuhusu Mbio za Hisani za NMB Marathon, Spika Dk. Tulia aliipongeza benki hiyo kwa namna ilivyotambua changamoto inayolikabili kundi la kinamama nchini, ambao wanateseka kwa Fistula, ambayo inaghjarimu kiasi kikubwa cha pesa kujitibu na kwamba yeye na wabunge watajisajili kushiriki ili kuchangia kiasi kilichokusudiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles