30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 17, 2024

Contact us: [email protected]

Watoto 700,000 kupatiwa chanjo ya Polio Simiyu

Na Derick Milton, Simiyu

Jumla ya Watoto 748,235 wenye umri chini ya miaka mitano mkoani Simiyu wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya Polio, kwenye awamu ya tatu ya chanjo hiyo ambayo itaanza kutolewa Septemba 1, hadi 4, mwaka huu.

Mratibu wa chanjo mkoa, Betrice Kapufi amesema kuwa maandalizi ya utolewaji wa chanjo hiyo yamekamilika kwa asilimia 100, ambapo jumla ya vituo vya kutolea huduma za Afya 1,668 vimendaliwa kutoa huduma hiyo.

Kapufi amaesema kuwa hiyo itatolewa katika maeneo yote ya kutolea huduma za Afya mkoa mzima kwenye halmashauri zake zote sita, ambapo maeneo ambayo vituo viko mbali vitaanzishwa vituo vya muda wa watoa huduma watakuwepo.

Amesema kuwa utolewaji wa chanjo hiyo ni mwendelezo wa kampeini mbili ziliopita, ambazo mkoa wa Simiyu ulifanikiwa kuvuka malengo ambayo yalikuwa yamelengwa ambapo chanzo ya kwanza ilitolewa Mei 18, 2022 hadi Mei 21, 2022.

Amewataka wananchi wote wenye watoto chini miaka mitano kuhakikisha wanakwenda katika vituo vya kutolea huduma za Afya vilivyopo karibu nao, kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo hiyo muhimu.

“Chanjo hii ni muhimu sana kwa watoto katika kupata kinga, tunawaomba wananchi wote kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya kwa ajili ya kupeleka watoto wao wapate chanjo hii,” amesema Kapufi.

Mshauri kutoka Shirika la Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk. Gerald Maro amesema kuwa katika awamu hii ya tatu, zoezi la utolewaji wa chanjo hiyo litafanyika zaidi nyumba kwa nyumba.

Amesema mbali na chanjo hiyo kutolewa kwenye vituo vya Afya zaidi, lakini wameweka nguvu zaidi zoezi kufanyika nyumba kwa nyumba ambapo watoa huduma watalazimika kuwafuata watoto majumbani.

“Katika kampeini ambazo zimepita mkoa wa Simiyu umefanya vizuri zaidi, ambapo kampeini ya awamu ya pili mkoa ulivuka lengo la asilimia 100 ukachanja hadi asilimia 121.

“Kampeini hii itafanyika zaidi nyumba kwa nyumba, ni kampeini maalumu ya house to house ( nyumba kwa nyumba) watoa huduma tayari wamewekwa katika makundi kuhakikisha wanatembelea nyumba kwa nyumba,” ameongeza Dk. Maro.

Mkuu wa Mkoa hu,o Dk. Yahaya Nawanda, amewataka wahusika wote katika chanjo hiyo kuhakikisha zoezi linatekelezwa kwa ufanisi, kwa kuhakikisha kila nyumba yenye mtoto inafikiwa na anapata chanjo.

Dk. Yahaya ameongeza kuwa mkoa wa Simiyu lazima uwe wa kwanza kitaifa katika kutekeleza zoezi hilo la chanjo ya Polio, kwa watoto wote ambao wanatajariwa kupewa chanjo kuhakikisha wanapatiwa ipasavyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles