25.1 C
Dar es Salaam
Thursday, May 2, 2024

Contact us: [email protected]

Watendaji wahimizwa kuongeza kasi utekelezaji wa Mradi wa AFDP

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene amehimiza kuwa na vikao vya uratibu vya pamoja kati ya wizara na taasisi zinazotekeleza mradi wa AFDP ili kuongeza kasi ya utekelezaji wake.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Dk. John Jingu akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, George Simbachawene katika kikao na watendaji wa TAFICO. 

Simbachawene ametoa rai hiyo jana alipotembelea Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) Kigamboni jijini Dar es Salaam ambalo linatekeleza programu ya kuendeleza kilimo na uvuvi katika mradi wa AFDP unaoratibiwa na wizara yake na kutekelezwa na Wizara za Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo na Wizara ya Uchumi wa Bluu na Uvuvi – Zanzibar.

Amesema programu AFDP ni ya miaka sita kuanzia 2021/2022 hadi 2027/2028 ambayo itagharimu jumla ya Dola za Kimarekani milioni 77.4 (Mkopo toka IFAD USD milioni 58.8; Serikali USD milioni 7.7; Sekta Binafsi milioni 8.4 na Wananchi USD milioni 2.4).

“Mradi huu wa uchumi wa bluu ukisimamiwa vizuri utaibua shirikia la TAFICO na utaibua uchumi wa biashara ya uvuvi zinazofanywa na sekta binafsi.

“Lazima tutengeneze kikosi kazi kitakachokuwa kinaashughulikia changamoto zinazojitokeza kutoka taasisi moja kwenda nyingine pamoja na wizara moja kwenda nyingine katika utekelezaji wa mradi.

“Eneo hili linaloshughulikiwa na shirika la TAFICO linaenda kujibu ahadi za ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020-2025,” amesema Simbachawene.

Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Dk. John Jingu amesema mradi huu ni mradi mkubwa sana na ni mradi wa kimkakati.

“Tuone namna ambavyo tutautekeleza huu mradi kikamilifu, spidi na kazi ya utekelezaji wa mradi bado hairidhishi,” amesema Dk. Jingu.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa TAFICO, Esther Mulyila akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, George Simbachawene vifaa vya shirika katika Gati la TAFICO lilopo kigamboni.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la TAFICO, Profesa Yunus Mgaya amesema wanalichukulia shirika la TAFICO kama shirika la kimkakati hasa katika dhana ya kutekeleza uchumi wa blue.

“Shirika linajukumu la kuwasaidia wavuvii wadogo wadogo hasa katika kunyanyua  vipato vyao, kuwawezesha kuhifadhi mazao yao ya uvuvi kuingia ubia na wananchi mbalimbali katika shughuli za uvuvi bahari kuu,” amesema Prof. Mgaya.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, George Simbachawene akitazama eneo la Gati la TAFICO.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles