25.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

TACAIDS yawaita wadau kuchangia Mfuko wa UKIMWI -ATF

*Yasema Kilichallenge imeleta mafanikio mazuri

*Yakusanya Sh bilioni moja

Na Nadhifa Omary, Kilimanjaro

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amewapongeza wapanda Mlima Kilimanjaro kupitia Kampeini ya Kilimanjaro Challenge Against HIV and AIDS kwa moyo walioonesha katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI nchini.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai akipewa taarifa ya huduma za VVU na UKIMWI zilizokuwa zinafanyika kuanzia Julai 15 hadi Julai 21, wakati wa Kampeini ya kupanda Mlima,kupitia Kilichallange Against HIV and AIDS 2022 kutoka kwa Dk. Didas Minis Mratibu wa UKIMWI wa Wilaya ya Hai. Mkuu wa Mkoa aliambatana na viongozi mbalimbali wa kitaifa pamoja na wadau. 

Akizungumza katika hafla ya kuwapokea wapanda mlima 52 na waliozunguka mlima amesema kwauthubutu kupanda mlima Kilimanjaro hadi kileleni tayari ni ushujaa wa kuigwa kwani ni mchango mkubwa katika kuhakikisha kampeini ya Kili challenge 2022 inafanikiwa.

Kagaigai ameongeza kuwa pamoja na malengo mengine ya kupanda mlima kupitia killichallange lakini bado ni kuunga jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kukuza utalii wa ndani kupitia vivutio vya utalii vya ndani ikiwemo mlima Kilimanjaro.

“Nawapongeza waratibu wa kampeini hii Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) ambao walikuja na wazo hili ambapo wameweza kupandisha watu 52 kwa mara moja, huu ni mwanzo mzuri kwani najua tangu ugonjwa wa Uviko-19 ulipoingia nchini mpango huu ulisimama kwa muda, na sasa mmerejea naamini fedha zinazopatikana zitakuwa na manufaa makubwa kwa walengwa,” amesema Kagaigai

Dk. Leonard Maboko akizungumza na wananchi walioshiriki hafla ya kuwapokea  waliopanda Mlima Kilimanjaro kupitia kampein ya Kilichallange Against HIV and AIDS  2022 mara baada ya kuwapokea kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai na Kulia kwake ni Makamu wa Rais wa GGML, Saimon Shayo. 

Kagaigai ameongeza kuwa lengo kubwa la kutekelezwa kwa kampeni hiyo ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI ambapo kwa kupitia program hiyo wadau wanapata fursa ya kuchangia fedha na kufanya utalii katika mlima Kilimanjaro ikiwa ni pamoja na kujenga urafiki na ushirikiano na Mataifa mbalimbali kupitia Mlima Kilimanjaro, ambao wanajitokeza kupanda mlima kupitia kampeini hiyo.

Aidha, amefafanua kuwa kampeini hiyo inatoa fursa kwa jamii na wadau mbalimbali kutambua masuala mbalimbali yanayohusu VVU na UKIMWI pamoja kuoanisha changamoto mbalimba za VVU na UKIMWI zilizotambuliwa na serikali pamoja na mipango iliyoainishwa ya utekelezaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko akimpongeza, Elly Kombe baada ya Kupokea cheti cha Kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia Kampeini Kilichange Aginst HIV and AIDS 2022, anayeshuhudia kulia kwa Dk. Maboko ni Saimon Shayo Makamu wa Rais wa GGM, Kombe ni Mshiriki kutoka TACAIDS

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko amewataka wadau mbalimbali kujitokeza na kuona namna ambavyo wanaweza kubuni njia nyingine ya kuchangia katika Mwitikio wa UKIMWI kupitia vyanzo vya ndani kwani kwa sasa fedha za UKIMWI zinapungua kutokana na wafadhili kuwa na vipaumbele vingine.

“Nawaomba wadau wengine mjitokeze,mje tukae mezani tuone namna tunavyoweza kubuni njia nyingine zinavyoweza kusaidia kupatikana fedha za mwitikio wa UKIMWI kwa kupitia vyanzo vya ndani.

“Hii kili challenge imeleta manufaa mazuri sana ambayo tuliibuni kwa kushirikiana na GGM lakini bado kuna njia nyingine tukikaa chini pamoja tunaweza kupata njia nyingine nzuri pia zinazoweza kutuletea fedha na zikasaidia au kuchangia katika kumaliza maambukizi ya VVU,” amesema Dk. Maboko na kuongeza kuwa:

“Kwa sasa tayari serikali imefanya marekebisho ya sheria ya kodi ya Mwaka 2020 kuwa kila anayechangia katika Mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti UKIMWI(ATF) fedha yote aliyochangia inakatwa katika kodi yake ya mwaka, mfano mfanyabishara akichangia Sh milioni 50, basi inahesabika kama tayari umelipa kodi,” amesema Dk. Maboko.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemerry Senyamule akizungumza na hadhara iliyohudhuria hafla ya kuwapokea wapanda Mlima 52 walioshiriki Kampaini ya Kilichallange Angainst HIV and AIDS 2022, ambapo ilijumuisha wapanda mlima 24 na waliozunguka Mlima kwa kutumia Baiskeli 28.wanaomsikiliza kutoka kulia kwake ni Kagaigai Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko, akifuatiwa na Saimon Shayo Makamu wa Rais wa GGML  na aliyekaa mwisho ni Kaimu Rais wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Vedast Makota. 

Aidha, Dk. Maboko ameishukuru GGM kwa program hiyo kwani kupitia wapanda mlima kwa mwaka huu wameweza kukusanya Sh bilioni moja, ambazo zitakuwa na mchango mkubwa kwa ajili wahitaji wakiwemo watu waishio na VVU pamoja na watu wengine wenye uhitaji kulingana na utaratibu wa Mfuko wa Kilichallange.

Akizungumza katika hafla hiyo Makamu wa Rais wa GGML, Saimon Shayo amesema GGML ipo tayari kuunga jitihada zinazofanywa na serikali katika kuhakikisha Watanzania wanajikinga na maambukizi mapya ya VVU, ndio maana hata katika program hii pia kumefanyika zoezi la upimaji wa VVU, chanjo ya Uviko-19 pamoja na kupima magonjwa yasiyoambukiza.

Wapanda Mlima 52 wakicheza kwa furaha baada ya kurejea baada kupanda Mlima kuanzia Julai 15 hadi 21, kupitia Kampein ya Kili challenge Against HIV and AIDS 2022 ambapo 28 walizunguka mlima kwa kutumia baiskeli na 24 walipanda kwa miguu hadi kileleni lengo ni kukusanya fedha za mwitikio wa UKIMWI nchini.

“Kwa GGML zaidi ya wafanyakazi 85 tayari wamechanja chanjo ya Uviko-19 hii yote ni kuhakikisha tunajilinda sisi lakini tunailinda na jamii inayotuzunguka, GGML tupo tayari kuendeleza ushirikiano na serikali kwa kadri tunavyoweza,” amesema Shayo. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles